GET /api/v0.1/hansard/entries/229070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229070/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Mr. Moroto): Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nami niungane na wenzangu katika kushukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa Hotuba yake. Mambo mazuri yalisemwa na yetu ni kushukuru tu kwa mipango ambayo ilitolewa katika Hotuba hiyo. Hata hivyo, kusema ni tofauti na kutenda. Bw. Naibu Spika wa Muda, tuna matumaini makubwa kwa sababu tumeona kazi ile Serikali imekuwa ikifanya tangu ilipochukuwa hatamu za uongozi. Hapa Bungeni, iwe ni Serikali iliyopita ama hii iliyoko, hakuna mtoto. Hii ni kwa sababu ya jinsi watu wamekuwa wakifanya kazi. Wengine wetu ambao tunatoka sehemu kavu za nchi hii wakati mwingine tunamlaumu Mungu kwa kutuweka katika sehemu ambayo alituweka. Hata hivyo, sasa hivi tumeanza kuona kwamba karibu tuwe sawa na wananchi wengine wa nchi hii. Kwa muda mrefu tumekuwa tukizozana na majirani zetu, lakini kwa wakati huu mizozano imepungua. Ukichunguza vizuri utagundua kwamba asili ya mizozo hiyo ilikuwa ni ukosefu wa mahitaji ya kimsingi kama vile maji, matibabu, chakula na elimu. Ukosefu huo ndio ulitufanya tuanze kutamani vitu vya watu wengine. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kushukuru Wizara kadhaa za Serikali kwa sababu zinafanya kazi nzuri. Ningependa kuanza na Wizara ambayo mimi ni Waziri Msaidizi na inahusika na maswala ya magereza. Ningependa sana wale ambao waliwahi kufungwa jela wakati mmoja na hawajarudi huko tena warudi ndani kidogo ili waone tofauti iliyoko sasa. Hapo mbeleni, magereza yalikuwa ni mahali palipolaaniwa. Wafungwa wengi hawakuwa na matumaini ya kutoka huko na kujiunga na wenzao. Mara nyingi, ikiwa mtu angefungwa gerezani kwa miaka miwili ama mitatu, basi angetoka akiwa amepoteza mengi maishani. Lakini kwa wakati huu, ukiwatembelea akina mama huko Lang'ata utapata kwamba kuna wanafunzi wafungwa katika kidato cha kwanza. Kuna wafungwa ambao wanasomea taaluma mbalimbali kama vile maswala ya ICT na wanafunzwa na wafungwa wengine ambao ni walimu. Hawa, labda walipatikana na makosa fulani kisha wakafungwa jela na wanatumia ule ujuzi wao sasa kuwasaidia wenzao. March 28, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 219 Kuna mwalimu mmoja wa kike ambaye alikuwa anafunza Mombasa Polytechnic. Kwa njia moja ama nyingine alipatikana na makosa na akafungwa miaka minne. Mfungwa huyo anafanya kazi nzuri sana gerezani. Anawafunza wenzake huku naye akijiendeleza kimasomo. Wafungwa hawa wanafanya mitihani ya kitaifa ambayo inasimamiwa na Baraza la Mitihani (KNEC). Kwa hivyo, mtu anaweza kuingia gerezani akiwa mtu duni lakini anapofunguliwa anaweza kufanya kazi mbalimbali ambazo hangeweza kufanya alipofungwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, katika magereza yetu tuna madarasa ya wanafunzi wa darasa la Kwanza hadi la Nane. Madarasa haya ni ya wafungwa. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwachukulia vibaya wafungwa. Kuna watu ambao hufungwa miaka kumi na minne na wengine hata hufungwa milele. Wafungwa hawa ni binadamu na ni Wakenya kama sisi. Kwa hivyo, wakiwa gerezani wanaweza kupata fursa ya kusaidiana. Hivi karibuni tutaanzisha mpango wa kuwaruhusu wafungwa wa kiume kutembelewa na wake zao. Hii itawawezesha kuongeza idadi ya Wakenya. Badala ya kurudi nyumbani baada ya kufunguliwa na kupata watoto ambao hawajulikani ni wa nani, sasa tunataka kuhakikisha kwamba mfungwa anapofunguliwa na kurudi nyumbani anaungana na watoto wake. Ningependa vile vile kuwashukuru Mawaziri wanaohusika na Wizara za Maji, Elimu, Afya na Kawi. Nawashukuru wenzangu kwa kutambua kazi inayofanywa na Wizara hizi. Kila mhe. Mbunge ambaye amesimama kuzungumza hapa, amezitaja Wizara hizi. Ningependa kumwunga mkono mwenzangu ambaye alisema kwamba wakati wengine wanajaribu kufanya kazi kwa bidii, kuna wengine wanaoshughulika na mipango ya kuiangusha Serikali. Tabia hii imezua lawama hivi kwamba watu wanalaumiana sana. Jambo ambalo lilifanya Serikali ya KANU ikataliwe na raia si kwamba Rais mstaafu Moi alikosea, bali ni kwamba wale wasaidizi wake ndio walikosea. Vivyo hivyo katika Serikali iliyoko katika mamlaka sasa, hapakosi watu wa kuharibu. Kila mtu sharti achunguze anafanya nini. Wakati kiongozi wa taifa anapotoa ushauri wake, sharti tujue ni nini watu wengine wanafanya. Bw. Naibu Spika wa Muda, lawama bado zinaibuka kuhusu maswala ya ajira. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa ukilinganisha Serikali hii na ile iliyopita. Wakati huo ungepata watu kutoka kabila moja katika nafasi zote za kazi katika idara. Sasa hivi tunaomba makosa hayo yarekebishwe ili tuwe na matumaini ya kupata matokeo mema. Kuna Mswada ambao utaletwa hapa Bungeni ambao unanuia kupiga vita umilikaji wa silaha bila idhini. Mswada huo unapendekeza kwamba mtu akipatikana na bunduki ahukumiwe kifo. Katika nchi hii kuna watu wajanja. Unaweza kupita mahali kisha mtu akuwekelee bunduki ama ipatikane kwako kwa njia ambayo hukutarajia. Kuna mambo mengi ya kushangaza sana. Nakumbuka wakati Bunge hili likianza kazi kuna Mbunge mmoja ambaye alileta Hoja ya kusema kwamba wezi wa mifugo wafungwe milele. Tunajua kwamba si kila mtu ni mwizi. Kuna wale ambao wanaweza kupatikana na makosa ilihali si wakosaji. Ni muhimu tuchunguze mambo fulani ili tujue ikiwa yatatupeleka mbele ama yatatufanya tuzozane na wenzetu. Wakati tunawapongeza Mawaziri ambao wamefanya kazi nzuri na kuwalaumu wale ambao ni wazembe, hata ile Kamati inayohusika na ratiba ya Bunge sharti ifahamu kwamba kila jambo wanalofanya ni kwa niaba ya Wakenya wote. Kwa hivyo, Miswada ile inayohusu maswala ya usalama na elimu sharti iwasilishwe mapema ili Wabunge waijadili vilivyo. Ninaishukuru sana Wizara ya Elimu kwa sababu kwa wakati huu, kinyume na vile mambo yalikuwa hapo awali, wanafunzi wanaishi kwenye mabweni ya shule. Wazazi wanaohamahama na mifugo yao wakitafuta malisho sasa wanaweza kuwapeleka watoto wao katika shule za mabweni. Wiki iliyopita tulipatiwa pesa ambazo zitawasaidia watoto hawa kuendelea na masomo yao. Tungependa kuiombea Serikali yetu ili iendele vizuri. Tunawapa changamoto wenzetu katika Upinzani kuongea mambo ambayo yanaweza kujenga nchi. Kuna tofauti kubwa sasa hapa Bungeni kwa sababu kwa mara ya kwanza kuna Wabunge katika Upinzani ambao wamesema hapa 220 PARLIAENTARY DEBATES March 28, 2007 kwamba Rais alisema mambo ya maana katika Hotuba yake. Huo ni ukweli. Hii nchi ni yetu na tusipompa moyo kiongozi wetu, tutapiga kelele kutoka mwaka wa kwanza hadi wa mwisho. Nchi zinazozana ni majirani wetu. Sisi tumebarikiwa na Mungu kwa sababu ametupatia viongozi ambao wana nia nzuri ya kutuweka pamoja ili tuendelee vizuri. Waziri wa Mifugo na Ustawi wa Samaki hayuko hapa Bungeni, lakini hajafanya kazi ya kutosha. Ni lazima awatembelee wafugaji na kuhakikisha mifugo yao inashughulikiwa ipasavyo. Mwisho, ningependa kumshukuru Waziri wa Jinsia, Michezo, Utamaduni na Huduma za Jamii kwa sifa nzuri ambayo ameiletea nchi hii. Tangu kuteuliwa wake, nchi yetu imepiga hatua katika riadha na kandanda. Kwa mfano, Kenya ilifanya vizuri katika mbio za nyika. Hata yule bingwa wa mbio hizo kutoka Ethiopia ambaye mashabiki wengi walidhani angelishinda, alishindwa hapa nchini Kenya. Mimi nina furaha kubwa kwa sababu wakimbiaji wengi wa timu ya taifa ya wanariadha wametoka Wilaya ya West Pokot. Tulifurahi kujumuika na Wakenya wa tabaka mbalimbali. Haya yote yalifanyika kutokana na juhudi za Waziri anayehusika. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii."
}