GET /api/v0.1/hansard/entries/229108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229108,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229108/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii niseme maneno machache kuhusu Hotuba ya Rais. Natarajia kwamba hii itakuwa mara ya mwisho kuwa na hali ambayo mtu atakuja atoe Hotuba hapa kama Rais, halafu sisi tuendelee kujadiliana wakati yeye hayuko hapa kusikiza yale tunayosema kuhusu hiyo Hotuba, hata kama anasikiliziwa na watu wengine. Nasema hivi nikitarajia kwamba mwaka ujao, tutakuwa na Katiba mpya ya Kitaifa ambayo itaruhusu kuwa na Waziri Mkuu ambaye ataongoza shughuli za Kiserikali na ambaye atakuwa anawajibika kwa maneno anayosema katika Bunge. Sio hali ambapo mtu atakuwa anaandikiwa Hotuba na maofisa ama na Mawaziri ili asome, kisha sisi tubaki tukicheza ngoma wakati mpiga ngoma hayuko. Nikisema hivyo, pia nasema kulingana na kule tulikotoka kihistoria kama nchi, tunaweza March 28, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 231 kusema kwa ukweli kabisa kuwa hali ya sasa ni bora kuliko ilivyokuwa hapo awali."
}