GET /api/v0.1/hansard/entries/229110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229110,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229110/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Ukiangalia mambo yote yanayoendelea katika nchi kwa jumla, iwe ni upande wa demokrasia, uchumi au vile tunavyoendesha mambo yetu kama Taifa, tunaweza kukubali ukweli halisi, kwamba hali ni bora kuliko vile ilivyokuwa hapo awali. Kile tu tunachoweza kusema ni kwamba, hali ingeweza kuwa bora zaidi kama tungefanya mambo mengine vizuri zaidi kwa kuyazingatia na kuyatekeleza vizuri. Hata tukiikosoa Serikali, tunaikosoa kwa misingi kwamba wakati huu, kuna hali halisi ya hewa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ambayo inaiwezesha Serikali hii kuweza kufanya vyema zaidi kuliko vile ilivyofanya kwa hiyo misingi. Jambo la msingi kuzungumziwa ni kwamba kazi kubwa zaidi ya Serikali yeyote duniani ni kulinda uhuru wa kitaifa. Nawashukuru wale ambao wanasema kwamba wakati umefika wa kuwaepuka mabeberu, kwani ni watu wanaokuja na asali mdomoni na mkuki mkononi, chambilecho alivyosema Chairman Mao tse Tung wa Uchina. Kwa kweli, sisi tukiwa viongozi tukifikiri kuwa mambo ya nchi yetu yanaweza kutatuliwa na mabeberu na watu kutoka nje, basi tujue kuwa tutapotea."
}