GET /api/v0.1/hansard/entries/229160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229160,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229160/?format=api",
    "text_counter": 43,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ndile",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
    "speaker": {
        "id": 272,
        "legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
        "slug": "kalembe-ndile"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kabla sijaongea juu ya Hotuba ya Rais, ningependa kuchukua nafasi hii kukushukuru kwanza kwa kutambua kwamba Wabunge wanafanya kazi. Kuna watu wengine ambao wanafikiria tulichaguliwa kufanaya kazi hapa Bungeni peke yake. Hawajui kwamba tunafanya kazi nyingi sana huko nje. Lakini uliwakumbusha. Bw. Spika, Hotuba ya Rais ilikuwa na mambo mengi sana. Ningependa kusema kwamba labda mimi sielewi sheria. Bado ninajifunza. Lakini, nakumbuka kuna sheria ambayo tulipitisha hapa Bungeni! Tulisema kwamba zawadi kwa Wabunge inayopita Kshs10,000 ikabidhiwe kwa Bw. Spika. Wakati niliona gari lingine hapa nje, nilifikiri ni lako kwa sababu ni zawadi na thamani yake inazidi Kshs10,000."
}