GET /api/v0.1/hansard/entries/229162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229162/?format=api",
    "text_counter": 45,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ndile",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
    "speaker": {
        "id": 272,
        "legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
        "slug": "kalembe-ndile"
    },
    "content": "Bw. Spika, sijui ikiwa nilielewa vibaya, lakini nilisikia kwamba hilo gari linaloitwa \"nyundo\" ni zawadi. Nakumbuka Wakenya walioko ng'ambo walipiga kelele sana wakati Wabunge walinunuliwa magari na Serikali. Walisema Wabunge walipewa magari ya bure. Wakati wa ukame, nilitoa gari langu liuzwe lisaidie watu wangu. Watu wanaongea juu ya ufisadi Serikalini lakini hapa nje, kuna mambo mengi sana ya ufisadi. Tunaiomba Serikali iangalie mambo hayo. Wakati huo wa ukame huo, Rais alitangaza kuna janga la njaa hapa Kenya. Kulikuwa na picha mbaya za watu walioathiriwa na baa la njaa. Kule kwangu, watu walikufa kwa kula mahindi yenye aflotoxin. Lakini, kuna mtu ambaye alifikiria kulitwaa hilo gari langu. Ndiyo maana tunaiomba Serikali ichunguze jambo hilo. Baadhi ya watu wanaofanya biashara za simu ni wezi. Ni lazima wachunguzwe na waangaliwe vile wanavyofanay kazi. Bw. Spika, nilishangaa sana kusikia juzi watu wakimshtumu Rais juu ya mshahara tuliomwongezea. Lakini yeye mwenyewe alisema hataki kuongezewa mshahara. Lakini kuna mtu mwingine ambaye anataka uongozi wa nchi hii na ananunua gari la Kshs54 milioni. Mtu huyo anawania kiti cha Urais. Ni lazima watu waache kujificha. Tunaambiwa kuna wakati nchi ya Uganda ilikuwa na siasa mbaya. Ukienda kununua bidhaa za Kshs2 milioni, ni lazima ubebe magunia mawili ya pesa. Hata hakuna wakati wa kuhesabu! Unamtupia mtu magunia hayo na unamwambia: \"Nipe televisheni ile! Hizo ni Kshs2 milioni. Ikiwa kuna matatizo, niambie ile wiki ijayo. Nitakuja!\" Sijui ikiwa uaminifu kama huo unaweza kufika nchi hii yetu ya Kenya. Kinachowatatiza viongozi wetu ni kutoaminiana. Juzi, Mhe. Rais aliongea hapa na akasema kwamba anataka Katiba mpya. Mimi nilifikiria \"minimum reforms\" isipokuja, dunia itapasuka! Wakati niliangalia yale wanayoyasema, ni yale yale tuliyoyasema katika Katiba iliyopita. Wanasema wanawake wawe wengi hapa. Nakubaliana na hayo lakini, ni vizuri tuache nafasi za kung'ang'ania hapa Bungeni. Kama ni hivyo, hata Wabunge wawajibike kupata asilimia 50 + 1 . Wengine tulikuja hapa Bungeni tukiwa na kura March 27, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 115 10,000 na wenzetu na kura 8,000, 7,000 au hata 5,000. Mbona wewe uko hapa na ulipita na kura 2,000 ama 800? Ni lazima haya mambo yote yaangaliwe."
}