GET /api/v0.1/hansard/entries/229164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229164/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ndile",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
"speaker": {
"id": 272,
"legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
"slug": "kalembe-ndile"
},
"content": "Bw. Spika, nasema hivyo kwa sababu hapa kuna siasa za kujificha na kuwadang'anya Wakenya. Ni lazima sisi viongozi tuanze kuaminiana. Kwa mfano, kuhusu mambo ya uraia, nina dadangu ambaye ameolewa ng'ambo. Ikiwa yeye amekuwa raia huko, hawezi kuja huku kwa sababu yeye ni raia wa kule na hawezi kupata uraia wa hapa lakini ni dadangu. Hakuna mtu alikataa hilo jambo. Lakini hawa walisema kuwa eti sheria haisemi hivi, inasema kuwa wanawake watatahiriwa! Siamini kuwa hata sasa tukisema tunataka kubadilisha Katiba, ni nini itawekwa kwa vichwa vyao waseme ukweli. Ikiwa hawatasema ukweli, labda wengine watasema ukweli. Sisemi ni upande fulani, lakini wote wanajificha. Viongozi ni lazima tuwajibike na tuangalie ni nini kinaweza kuwasaidia watu wetu. Hata kama wamepewa zawadi kama za gari, tunataka kuona mhe. Kalonzo na mhe. Balala wakipewa hiyo Hummer wiki moja. Maskini rafiki yangu, Prof. Ojiambo, ambaye hawezi kununua Hummer, yafaa apewe aiendeshe wiki moja."
}