GET /api/v0.1/hansard/entries/229166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229166,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229166/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ndile",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
"speaker": {
"id": 272,
"legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
"slug": "kalembe-ndile"
},
"content": "Tukiendelea hivyo, hata mimi nitafikiria kama nitajiunga na ODM(K) nione kama nitapewa Hummer kwa sababu siwezi kuinunua. Ni lazima viongozi wetu waseme wanavyotaka kufanya. Nikizungumzia jambo lingine, watu wamewatumia vijana vibaya. Kama ningetumiwa vibaya, singekuja Bungeni. Niliomba kura kwa watu wangu nikitumia baiskeli. Hakuna mtu aliyesema kuwa nilikuwa naomba kura na kwa vile ninampinga mtu fulani yafaa nichomwe. Hata juzi nilijaribu kusema kuwa vile rafiki yangu mhe. Wamwere alifanyiwa si vizuri. Lakini nilisema kuwa si chama kinachofanya hivyo; ni watu. Watu wasifanye kitu na wasingizie chama. Kwa yale mambo nilifanyiwa huko Mwingi, sikuona chama cha ODM(K) pale. Ni watu walipanga! Niliwaona wahe. Musila na Kalonzo wakipanga!"
}