GET /api/v0.1/hansard/entries/229175/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229175,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229175/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ndile",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
"speaker": {
"id": 272,
"legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
"slug": "kalembe-ndile"
},
"content": "Nasema hivyo kwa sababu hao watu walisikika wakisema: \"Vile mwingine amesema, nimeweka sahihi, eti mhe. Ndile ameondolewa.\" Ni hao watu! Ni lazima siasa zetu ziwe za kukubaliana kimawazo. Niliwasamehe na sitaki kurudia hayo maneno lakini sitaki kuona vijana wakitumiwa vibaya. Vijana ni lazima waanze kufunzwa. Mimi nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa ukoo wetu nikiwa na miaka 28. Nilimuuliza baba yangu ni kwa nini wazee walinichagua na kama ningeweza kutatua matatizo kama vile baba yangu angekosana na mkewe. Waliniambia nisijali kwa maana siku kama hiyo ikifika, watatafuta wazee wa kusuluhisha hayo mambo, maana ni makubwa kuliko mimi, ijapokuwa walikuwa nyuma yangu. Ni wangapi hapa ambao wako tayari kuwafunza viongozi wadogo njia ya kuwajibika? Ni wangapi hapa wataamka na kumaliza vita? Ni lazima tufanye hivyo Bungeni. Mara nyingine, mimi hujiuliza kama hili ndilo Bunge nilikuja kuwakilisha watu wangu wa Kibwezi, ama hili ni Bunge gani? Kwa maana utamsikia mtu akisema jambo fulani na kesho yake anasema jambo lingine. Kesho watakusengenya halafu wakane. Ni lazima tuanze kukua na kukua ni kuwajibika kama tulivyosema. Ikiwa ni kura, mwishowe tutaenda kwa debe. Watu wetu wataenda kwa debe na mtu atakuwa pale peke yake na kupiga kura yake. Lakini akijiuliza ni kwa nini alimuumiza mwenzake sikio, hatajua. Bw. Spika, hii nchi ikiendeshwa vizuri kwa uongozi, itapiga hatua. Juzi, watoto wetu walikuwa wakifukuzwa kutoka shuleni lakini sasa hawafukuzwi. Ikiwa Mawaziri wengine hawangekuwa wakipiga kelele kwa miaka miwili na kusema Bw. Kibaki aondoke, tungekuwa mbali. Tungekuwa na elimu! Hata nilikuwa nimeanza kuwaambia vijana kwamba hawatakuwa na shida. Kuna wengine ambao hawawezi kuoa au kuolewa. Wanashindwa wakioa wake watawapatia nini au waume watawapa nini kwa sababu ya shida. Nilikuwa nimeanza kuwaambia wale walikuwa wakifikiria kuwa uchumi hautakuwa mzuri, wana bahati na waoe na kazi yao itakuwa ni kuzaa. Hawangekuwa na kazi nyingine, maana Serikali ingewalipia karo za shule. Hiyo haikufanyika kwa sababu wakati wote viongozi wetu wakiona mtu anafanya vizuri, wanataka kutafuta mbinu za kumharibia. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}