GET /api/v0.1/hansard/entries/229302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229302,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229302/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nikizungumza kutoka sehemu hii ya Bunge hili, wengi wanashangaa na wanauliza ni kwa nini ninafanya hivyo, ilhali wao hawashangai wanapotoka sehemu ya kulia na kwenda sehemu ya kushoto. Ni lazima kila Mbunge na chama kipewe haki ya kutekeleza demokrasia itakavyo. Sio kwamba, wengine wana ruhusa ya kwenda sehemu ya kushoto na wengine hawana ruhusa ya kwenda sehemu ya kulia ya Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningetaka kuchukua fursa hii kumpongeza Rais na kuunga mkono Hotuba yake, iliyotoa mwongozo wa sera na sheria, kwa sababu, siasa sio porojo bali ni sera na sheria."
}