GET /api/v0.1/hansard/entries/229304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229304/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Katika Hotuba yake, Rais aligusia swala la uhalifu au sheria zilizoidhinishwa, ikiwemo uhalifu wa kiuchumi, usimamizi wa mali ya umma, maadili mema ya wafanyikazi na ubinafsishaji wa mashirika yasiyo ya Serikali. Haya yameboresha hali ya maisha ya Wakenya na uchumi wa taifa hili. Hali hii imechochea uwekezaji zaidi wa rasilmali za nje katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ama kwa hakika, huu ndio ufanisi na usawa ambao Wakenya kwa mara ya kwanza katika miaka 40 wameanza kusherehekea leo! Ninasema haya kwa sababu kuna mtiririko wa rasilmali ya taifa katika mashinani, zikiwemo pesa za CDF, pesa za barabara, pesa ya mabaraza ya wilaya, pesa ya vijana, na hivi karibuni tunatarajia pesa ya akina mama. Huu ndio usawa na ufanisi. Vijana wetu wana sababu ya kusherehekea, kwa sababu wanapata elimu bila malipo katika shule za msingi. Hapo mbeleni, watoto wa shule za msingi walikuwa 6,100,000 na leo wamefika 7,600,000. Hili ni dhihirisho kwamba, kutoa elimu bila malipo ni faida kubwa kwa watoto wetu na tunawatayarisha ili wajiandae kwa jukumu ambalo liko mbele yao. Sikatai, kuna changa moto, yakiwemo maswala ya kuongeza walimu na karakana katika sekta ya elimu, lakini hatua iliyochukuliwa na Serikali inapaswa kuungwa mkono."
}