HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229306,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229306/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "138 PARLIAMENTARY DEBATES March 27, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna hazina ya vijana. Maeneo ya Bunge 210 yamepokea Kshs210 milioni. Hivi karibuni, zaidi ya Kshs7 milioni zitapeanwa kwa vikundi vya vijana. Pesa hizi zitawawezesha vijana wetu kujinufaisha na kujiboresha katika nyanja ya kibiashara. Kuna vipofu na viziwi ambao hawawezi kusikia, kuona au kuzungumza juu ya haki zao. Ukizungumza juu ya sera au sheria, unaambiwa kuhusu ufisadi. Kumaliza ufisadi siyo rahisi kama kunywa kahawa ambayo itakuchemsha damu mara moja; kumaliza ufisadi kunahitaji karakana, mikakati, sera, sheria na uwiano. Tukisimama pamoja, tutafaulu kupambana na ufisadi. Tukingojea Rais Kibaki amalize ufisadi katika nchi ya Kenya, itakuwa vigumu. Ni lazima kuwe na ushirikiano, uwiano, sera na sheria zitakazowezesha nchi kupambana na ufisadi. Bw. Naibu Spika wa Muda, leo nazungumza kwa furaha kubwa. Nilisimama katika Bunge hili miaka minne iliyopita kuzungumza juu ya giza kutokana na ukosefu wa nguvu za umeme. Kwa mara ya kwanza, tarafa za Madogo na Garsen katika Wilaya ya Tana River zimepata nguvu za umeme. Sina budi kuipongeza Wizara inayohusika na Rais kwa kuweka mikakati hiyo, ili watu wa Tana River wanufaike kama Wakenya wengine. Lakini wasiokuwa na macho ni vigumu kuona maendeleo kama hayo. Kutoka mwaka wa 1963 hadi 2002 - karibu miaka 40 - Serikali ilitumia Kshs6 bilioni. Lakini katika miaka minne ya utawala wa hii Serikali, kiasi cha Kshs7 bilioni kimetumiwa katika usambazaji wa nguvu za umeme mashinani. Leo, kwa vile kuna nguvu za umeme mashinani, kuna biashara ndogo ndogo na vijana wetu wamepata fursa ya kujiajiri wenyewe. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumzia maswala ya Katiba mpya. Wakati nilizungumzia juu ya ufisadi, nilisema ni sharti tuwe na uwiyano. Vile vile, tukija kwa Katika mpya, ni sharti tuwe na uwiyano. Ni lazima tuwe na mazungumzo. Ni lazima watu wakae, wazungumze na wakubaliane. Siyo mtu mmoja kutoa maongozi ya vile atachukua uongozi kupitia mlango wa nyuma. Sio hivyo. Sheria ya nchi ni sheria ya nchi! Siyo sheria ya chama au mtu fulani. Sheria ya nchi ni ya nchi. Ni lazima Wakenya waletwe pamoja, wakae pamoja, wazungumze na wakubaliane. Mhe. Rais alipozungumza hapa alitoa mwongozo juu ya Katika mpya na tunamuunga mkono. Jana, tulitangaza kamati yetu. Tunangojea kamati kama hiyo ibuniwe upande huo ili tukae na tulete sheria tunazopendekeza. Mbunge mmoja alizungumzia juu ya hali mbaya katika sehemu kame hapa nchini. Ni kweli hali ni mbaya katika sehemu kame. Ni kweli umaskini umetanda katika sehemu kame. Lakini siyo kama miaka 40 iliyopita. Leo, kuna mtiririko wa rasilmali ya kitaifa katika sehemu kame. Kwa mfano, kuna madarasa 90 mapya katika sehemu ya uwakilishi bungeni ya Bura. Kwa miaka 40 iliyopita, miradi kama hiyo ilikuwa wapi? Sehemu kame zina shida. Zimedhulumiwa kwa miaka 40. Ni vigumu kuonda dhuluma kwa muda wa miaka minne. Lakini, mikakati ya kuondoa dhuluma katika sehemu kame imeanzishwa na Serikali hii. Mbunge mmoja alikosoa na kupeana mfano wa sera za nchi za nje. Bila shika, sera zetu za ndani ni nzuri. Hata wao wamekubali. Hotuba hii ya Rais ni ya mwisho katika Bunge la tisa. Lakini siyo ya mwisho katika Bunge la Kenya. Kwa vile tuna hakika atarudi tena, ataweka sera za nje katika hotuba zake. Kwa hayo machache, nasimama kumuunga mkono na kumpongeza Rais kwa Hotuba yake."
}