GET /api/v0.1/hansard/entries/229392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229392,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229392/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii na mimi nichangie Hotuba ya Rais. Ningetaka kuisifu Serikali sana kwa kazi nzuri ambayo imefanya. Lakini pia, ni vizuri kukumbuka kwamba mgema ukimsifu, ni rahisi sana kuitia tembo maji. Kwa hivyo, ningetaka kusema machache kuhusu yale ambayo kama tutayafanya, yataweza kutusaidia zaidi. Bw. Spika, furaha kubwa ya Serikali inaonekana ni kwamba uchumi umefufuka na unaendelea kukua kwa asilimia 6 kwa mwaka. Ningetaka tu kuikumbusha Serikali ya kwamba kuvua numbi si kazi; kazi ni magawiyoni! Ni lazima kilichokuwa kikuliwe na wote. Ningetaka kuongeza ya kwamba uchumi ambao utamsaidia mtu mmoja kuchuma Kshs2 billioni kwa mwaka wakati wengine hawapati mkate wao wa kila siku, kidogo uchumi huo umepotoka na ni lazima uwekwe laini. Katika kipindi kinachobaki cha Bunge, ni matumaini yangu ya kwamba Serikali March 22, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 71 itakumbuka kutekeleza Hoja zote zile ambazo zimepitishwa na Bunge hili lakini hazijatekelezwa. Nakumbuka ya kwamba kuna Hoja moja nilioleta hapa Bungeni kuhusu kurudishiwa mashamba wale ambao walinyang'anywa mashamba yao wakati wa vita vya kikabila. Mpaka sasa watu hao hawajarudishiwa mashamba yao. Nadhani ni hila mbaya kwa upande wa Serikali kutaka kungojea mpaka kipindi chake kiishe kabla ya kutimiza ahadi hii iliyomo katika Hoja. Bw. Spika, pia nakumbuka kuna Hoja ingine iliyopita katika Bunge hili kuhusu kulipwa kwa fidia wale watu ambao waliteswa na kufungwa bure na Serikali ya KANU katika miaka ya 1980s na 1990s tangu Uhuru. Matumaini yangu yalikuwa ya kwamba Hoja hiyo ingetekelezwa mara moja lakini imelaliwa. Sijui imelaliwa kwa sababu Serikali imegairi, au imelaliwa kwa sababu Serikali inafikiria ya kwamba hakuna watu walioteswa. Sijui! Lingine ningetaka kutaja ni kwamba ugamvi wa rasilimali wa kikabila umeadhiri sana wilaya zingine kama vile Wilaya ya Nakuru. Nafikiria hili linatokea kwa sababu maeneo yasiyo makazi ya kijadi yamekuwa yakibaguliwa. Labda Wabunge wengi hawajui ya kwamba katika Wilaya ya Nakuru, hatupewi Waziri. Hatujapewa Waziri tangu mwaka wa 1966. Sijui ni kwa nini kwa sababu kuna wanasiasa shupavu, tunapiga kura kama sehemu zingine za nchi lakini hatupewi Waziri."
}