GET /api/v0.1/hansard/entries/229395/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229395,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229395/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assitant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Spika, lingine ambalo labda mheshimiwa hana habari nalo, wilaya kama ya Nakuru haipewi nyadhifa kama zile za District Commissioner (DC), Provincial Commissioner (PC), Permanent Secretary (PS), balozi na hata wakurugenzi wa makampuni makubwa. Mpaka wa leo, sijaelewa ni kwa nini jambo hili halifanyiki. Nimelifanyia utafiti; najua ninachoongea na ninajua ya kwamba ninasema ukweli mtupu. Tunataka jambo hili lirekebishwe. Wengine watasema ya kwamba tunanyimwa kwa sababu kura zetu zinasemekana ziko mifukoni na kwa hivyo hakuna haja ya kubembelezwa. Lakini sioni kwa nini kama kura zetu ziko mifukoni mwao, wasitushukuru kwa kutupa kazi zile ambazo wanapea wale ambao wanataka kuwashawishi wawape kura? Bw. Spika, majuzi tumeambiwa kwamba idadi ya watu maskini humu nchini imefika 27 milioni. Mimi nilidhania kwamba Rais Kibaki angetangaza jana kwamba umaskini ni baa la taifa lakini hakufanya hivyo. Isitoshe, umaskini huu umewafanya watu 27 milioni wasiwe na uhakika wa kupata chakula chao cha siku. Hii ni kuonyesha kwamba labda umaskini sasa umekuwa tatizo kubwa nchini na lazima utafutiwe suluhisho na uwekewe mikakati inayofaa. Kwa sasa, naona ni kama Serikali inafikiria kwamba umaskini ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa kupitia fadhila za matajiri. Hilo katu haliwezekani na halijawezekana. Sharti Serikali iweke mikakati kamili ya kumaliza umaskini ikiwemo mipango ya kuongeza Hazina ya Maendeleo ya Uwakilishi Bungeni (CDF) pamoja na hazina ya LATF. Aidha ni muhimu maskwota wapatiwe mashamba kwa sababu watu wengi wanamiliki mashamba mengi ambayo hawayatumii. Wengine wana ekari 400,000 ya mashamba na sijui wanataka kuyafanyia nini. Hata swara wamepewa ekari nane kule Laikipia wakati ambapo watu wetu wanakufa kwa kusongamana katika miji ya mabanda kama vile Mathare na Kibera. Bw. Spika, umaskini unaweza kupigwa vita pia kwa kuwasaidia watoto maskini kupata elimu, nafasi za kazi zitafutwe kwa kila namna, bei za bidhaa lazima zisimamiwe na mshahara wa chini lazima uinuliwe. Hatua kama hizi zitasaidia sana. Jambo jingine ambalo ningependa kugusia ni kuhusu ufisadi. Ufisadi hauwezi kuisha bila 72 PARLIAMENTARY DEBATES March 22, 2007 kupigwa vita. Kwa maoni yangu, inaonekana kama kwamba ufisadi umesamehewa bila ya kusema. Hii ni kwa sababu hatuoni wafisadi wakifungwa. Hatukuambiwa hatima ya kashfa za Goldenberg na Anglo Leasing. Hatukuambiwa! Ningetaka kumsikia Rais akisema kwamba mwaka huu tutapata ufumbuzi kuhusu kashfa hizi mbili. Kutoka upande wa Serikali, kile tunachopata ni kimya tu. Ufisadi kule mashinani haushughulikiwi vilivyo. Ningependa kuona ufisadi ukishughulikiwa kule Subukia lakini bado haijawa hivyo. Kuna machifu niliomba wafukuzwe kazi kwa sababu ni wafisadi lakini nikapuuzwa. Bw. Spika, tunaona nchi za kigeni zikiwakataza wafisadi kusafiri kwa nchi zao, lakini hapa kwetu wafisadi wanatafuta kuwa Rais na Wabunge. Nashindwa kuelewa ni kwa nini nchi za kigeni zifikirie juu ya ufisadi kuliko sisi wenyewe? Wapiga firimbi katika nchi hii bado hawalindwi wala hatujapitisha sheria za kuwalinda. Najua kuna wafanya kazi 11 wa hoteli ya Grand Regency ambao walifutwa kazi miaka mitatu iliyopita na hadi leo hawajaruhusiwa kurudi kazini kwa sababu polisi mmoja huwapa ulinzi ilhali mwingine hutoa amri ya kupinga hilo. Ikiwa tunasema kwamba tunapiga vita ufisadi, wale wanaosaidia Serikali kupiga ufisadi vita, lazima wasiadhibiwe kwa kufutwa kazi. Bw. Spika, uliongea juu ya ukabila katika hotuba yako. Ninakubaliana nawe kwamba ukabila ni tatizo kubwa na ndilo litakuja kuumbua taifa hili. Hata hivyo, ninataka kukusahihisha kidogo. Ulisema kwamba kuna \"demokrasia ya kikabila\", lakini mimi ningependa kuongeza kwa kusema kwamba tuna \"udikteta wa kikabila\"."
}