GET /api/v0.1/hansard/entries/229397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229397,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229397/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assitant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": "Udikteta huu unapuliziwa hewa na vyama vya kikabila. Hata sisi ambao tunapinga ukabila tunaitwa wasaliti na watu wanakuja kutuchomea kwetu. Mhe. Mbunge mzima aliongoza jeshi la kuja kutuchoma eti kwa sababu tumejiunga na chama kingine. Watu ambao wanaamini kwamba wataelekeza nchi hii kwingineko tofauti na kule tulikoelekezwa na KANU - naongea kuhusu wafuasi wa chama cha NARC(K) - lazima wakifanye kile kilichofanywa na Serikali ya KANU wakati wa enzi ya giza. Ni jambo la kushangaza kwamba kila siku tunashinda tukihubiri kuhusu majimbo. Majimbo hayo ndiyo yatamaliza nchi hii na lazima ieleweke hivyo."
}