HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229513,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229513/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nitoe maoni yangu kuhusu Hotuba ya mhe. Rais ambayo alitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge hili juzi. Nina furaha kwa sababu wakati huu akina mama pia wamekumbukwa. Ninatumaini ya kwamba hela hizi ambazo zitatengwa kuwasaidia akina mama kufanya biashara ndogo ndogo hazitawekewa vikwazo vingi kama vile pesa za vijana zilivyowekewa. Mara kwa mara, wakati vijana wetu ama kina mama wanapoenda kuchukua mikopo kutoka kwa benki za humu nchini, hawapati hela zo zote za kuwasaidia kufanya biashara ndogo ndogo. Vile vile, nimeona kuwa ikiwa kitengo hiki cha akina mama kitakuwa kama kile cha vijana, kitaleta balaa. Nusu ya pesa hizi zimepatiwa benki zile zile ambazo zinatoa mikopo na riba ya juu. Kitengo kikubwa cha pesa hizi kimekwenda kwa Kenya Women Finance Trust (KWFT) na benki ya K-Rep. Mashiriki haya yote yanafanya kazi kufuatia sheria za benki na sio rahisi kwa vijana kupata pesa hizo ambazo ziko katika benki hizo. Lakini ningependa kumshukuru mhe. Rais kwa kuwakumbuka akina mama. Ikiwezekana, sheria za kuwasaidia kina mama, zinafaa kufanywa nyepesi ili akina mama wengi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye vikundi waweze kupata pesa kwa njia rahisi ijapokuwa riba iko juu sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, ijapokuwa mhe. Rais amezungumza juu ya asilimia 30 ya akina mama kupata kazi nchini, ukisoma magazeti, haswa gazeti la Serikali, utaona kwamba akina mama wanaachwa nje na hawahesabiki. Kazi zile nyingi hutolewa na Mawaziri ambao wamechaguliwa na mhe. Rais. Ninashangaa kwamba mkono wa kulia na wa kushoto haizungumzi lugha moja. Mhe. Rais anasema kuwa akina mama ni lazima wapate asilimia 30 ya kazi nchini, lakini Waziri katika Serikali yake hatimizi jambo hili. Ningependa kukumbuka kisa cha hivi juzi ambapo tuliona mama aliyekuwa Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Kenya akitengwa kwa misingi ya kikabila. Kabla ya hivyo, Waziri wa Fedha alikuwa anataka tubadilishe sheria ili wapate kuwa na mwenyekiti mkuu wa Benki Kuu ya Kenya, lakini tuliikataa sisi. Baada ya kuikataa sheria hiyo, kwa maana alikuwa ameitenga kazi hiyo kwa rafiki yake ambaye amempatia wadhifa wa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, sasa hivi tunaambiwa kwamba mama huyu hafai kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya kwa sababu hana kisomo kama 100 PARLIAMENTARY DEBATES March 22, 2007 kile cha wale wengine. Ikiwa alikuwa Naibu wa Gavana, inawezekanaje kuwa hafai kuwa Gavana? Kwa hivyo, akina mama wana masikitiko makubwa sana kwa hatua hiyo. Ijapokuwa mhe. Rais amejaribu kufanya kazi yake, maswala kama hayo yanamharibia sifa kwa akina mama. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumza kuhusu janga la Ukimwi. Mhe. Rais alitaja kwamba pesa nyingi zimetengwa ili ziwasaidie walio mashinani kupambana na makali ya janga hilo. Ukweli ni kwamba mhe. Rais hajaelezewa ukweli wa mambo! Kwa muda wa zaidi ya miaka miwili, hakuna pesa ambazo zimetoka katika National AIDS Control Council (NACC) kwenda mashinani. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumza juu ya maswala ya maendeleo ya Mkoa wa Pwani. Mhe. Rais alisema kuwa Mkoa wa Pwani ni moja ya maeneo ambayo yamewekwa katika mradi wa kushugulikia sehemu kame za nchi hii. Mhe. Rais alisema kwamba kuna Kshs8 bilioni ambazo zimetengwa na, kwa wakati huu, zinasaidia katika miradi mbali mbali. Kusema ukweli, Kshs8 bilioni ni pesa nyingi sana. Ikiwa zinatumika kufanya miradi katika mkoa huo, tungekuwa tukiona kazi hiyo. Sijui ikiwa mhe. Rais anaelezewa ukweli wa mambo. Lakini muda unavyozidi kwenda, labda atajua ukweli wa mambao kwa sababu hatujaziona hizo Kshs8 bilioni. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuikumbusha Serikali hii kwamba Mkoa wa Pwani unachangia kitengo kikubwa sana katika uchumi wa nchi hii. Bw. Tuju amezungumzia kuhusu swala la utalii. Biashara nyingi za utalii ziko Mkoa wa Pwani. Mbuga za wanyama pia zinachangia pakubwa katika uchumi wetu. Madini ambayo yako pwani na bandari ya Mombasa inachangia kitengo kikubwa sana cha uchumi wetu. Je, watu wa pwani wanapata ama hawapati haki yao? Ukweli ni kwamba watu wa pwani hawana raha na hawapati haki yao. Labda mhe. Rais hana habari hiyo. Lakini mwaka huu ni wa siasa na hivi karibuni, tutajua ukweli wa mbivu na mbichi kwa sababu wananchi wa Mkoa wa Pwani wamezoea kutumiwa kama muhuri. Tumechoka kutumiwa kama muhuri! Tumepewa ahadi ya kwamba maskwota watatengewa maeneo yao. Tunangoja tuone ikiwa ahadi hiyo itatimizwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kabla sijamaliza - namwona Bw. Tuju ameondoka, ningependa kumkumbusha kwamba huwezi ukafananisha shati na ua ambalo ukilichuma mchana, huwa limenyauka jioni. Serikali ya NARC, kupitia kwa Rais Kibaki, wamejaribu kulitia matundu shati hilo na kulibandika viraka. Hatujafurahia kitendo hicho. Kwa wakati huu, si ajabu kwamba shati hilo linafanana na rangi ya machungwa kwa sababu wamelitia mashimo. Si ajabu kuwa kwa sababu shati hilo limegeuzwa rangi likawa la rangi ya machungwa, litawaonyesha mlango mwaka huu. Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}