GET /api/v0.1/hansard/entries/229525/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229525,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229525/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Capt. Nakitare",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii inayohusu Hotuba ya Rais. Hotuba yake ilikuwa kama fumbo kwa wale walio hai. Naishukuru Serikali hii kwa sababu, kwa miaka minne iliyopita, watu wameona matunda ambayo yalikuwa hayaonekani wakati wa utawala uliopita. Nashangaa kuwasikia baadhi ya Wabunge wakiikashifu Serikali hii, wakisema kwamba haijafanya chochote. Wengi wao walikuwa katika Serikali iliyotangulia. Kwa nini hawakuikosoa Serikali hiyo? March 22, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 103 Ningependa kugusia mambo ya usalama nchini. Namshukuru Rais kwa kufanya jitihada za kuleta amani kupitia mazungumzo. Yeye ni mtu mtulivu ambaye anasikiliza. Ningemuomba asisitize mambo haya katika ofisi yake. Tunafaa kuwakumbuka wale waliopigania Uhuru ingawa hawakutajwa katika Hotuba ya Rais. Nilikutana na Mzee Gitu Kahengeri ambaye alikuja kushuhudia kufunguliwa kwa Kikao hiki cha Bunge, ingawa hakuingia humu ndani. Alikuja kama mpiganiaji wa Uhuru wa Kenya. Kuna watu wengine pia ambao walipigania Uhuru wa Kenya. Kwa mfano, watu wa Dini ya Msambwa walipigana na wabeberu. Wengi wao waliuawa kule Malakisi. Ningeiomba Serikali hii iwakumbuke hao watu. Dini hiyo haikuwa kama lile kundi haramu la Mungiki. Wafuasi wake hawakuwa wakiwapiga watu. Naomba dini hiyo ifufuliwe. Dini hiyo ilisaidia katika kuyaunganisha makabila mbali mbali. Hawakuwa wakipigana kama baadhi ya jamii wanavyofanya sasa. Dini hii ilikuwa pia kule Mt. Elgon. Chief Tendet alikuwa akiwafundisha watu wake jinsi ya kukaa na wenzao kwa amani. Inasikitisha kwamba mambo yanayoendelea kule Mt. Elgon hayakugusiwa katika Hotuba ya Rais. Nawaomba, Bw. Magut, Bw. Wilberforce Kisiero na Bw. Kimkung washirikiane pamoja na Bw. Serut ili wakomeshe mauaji yanayotendeka kule Mt. Elgon. Kwa nini hawa watu wanatengana? Serikali imewapeleka askari katika sehemu hiyo. Je, askari hao watasaidia vipi kutatua mzozo katika sehemu hiyo? Watu wanaozozana wanafaa kukaa pamoja ili waafikiane. Wanaoumia ni watoto na akina mama. Ni ajabu kuona kwamba watu kutoka nchi jirani wanaingia humu nchini na kuchoma mimea, nyumba na kuwaua watu."
}