GET /api/v0.1/hansard/entries/229534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229534,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229534/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ni uchungu ambao unanifanya nizungumze hivyo kwa sababu watu wanakufa, hali watu wa Nairobi wanafanya mchezo, kama uliokuwako wakati wa vita vya kikabila. Hivi sivyo vita vya kikabila. Mimi naleta mambo haya ili ieleweke kwamba Serikali ina jukumu la kupatanisha watu. Hawa wazee niliowataja ni wazee wa mikoa; ni wazee wa ukoo wanaoweza kupatanisha watu. Sikusema kuwa ni wazee wanaopiganisha watu! Haya ndiyo mambo ambayo watu huyachukulia kwa wepesi bila kuelewa. Katika Hotuba yake, mhe. Rais aliweza kuleta mbwanda kwa akina mama. Sisi 104 PARLIAMENTARY DEBATES March 22, 2007 tulisomeshwa na akina mama ambao hawakwenda shule. Akina mama waliotuzaa walitusomesha kwa kuuza mboga, matunda na maziwa na hawakujua hesabu. Leo hii, ikiwa huu mradi wa akina mama utaanzishwa, je, hawa akina mama walioko sokoni wana elimu ya kutunza hizo pesa? Kwa hivyo, tunaihimiza Wizara ya Elimu iwaelimishe hawa akina mama kwa elimu ya ngumbaru ili waweze kupata njia ya kuweza kujimudu kwa kutumia hizo pesa. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo linalonifurahishwa haswa ni lile la wawekezaji wa raslimali yao hapa Kenya. Nafurahi huona kuwa Virgin Atlantic Airlines, ambayo ni kampuni ya ndege, imekubali kuwaleta watalii nchini moja kwa moja kutoka America mpaka Nairobi. Pia, tungependa tupate ndege ya kwenda moja kwa moja kutoka Uhispania kuja mpaka Nairobi ili ibebe mboga zetu waende kuwauzia wale watu. Haya ndiyo matunda ambayo Serikali ya Kenya imepata chini ya Rais huyu mpole ambaye hasemi. Sisi tunamwekea maneno mdomoni ili tumlazimishe aseme, na yeye mwenyewe yuko na ujasiri. Yeye ni tausi. Akipanua maua yake, kila mtu anajua. Na nitamwambia Mbunge mwenzangu kwamba tunda linatoka kwa maua. Maua ndio huja kwanza na yakikomaa, ndio tunda linatoka. Hiyo ndio jawabu ya mifumo ya hivi vyama vyenu. Tunda haliji kabla ya maua, bali maua huja kabla ya tunda. Kwa hivyo sasa, ule msemo unaosema kuwa maua hubadilika katika rangi ya---"
}