GET /api/v0.1/hansard/entries/229598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229598,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229598/?format=api",
    "text_counter": 28,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Awori",
    "speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
    "speaker": {
        "id": 290,
        "legal_name": "Moody Arthur Awori",
        "slug": "moody-awori"
    },
    "content": " Mr. Speaker, Sir, I beg to move the following Motion: THAT, the thanks of this House be recorded for the exposition of public policy contained in His Excellency's Presidential Address from the Chair on Tuesday, 20th March, 2007. Asante Bw. Spika. Nitachukua fursa hii kusema machache juu ya Hotuba ya Rais. Tumekuwa katika likizo kwa miezi mitatu. Nafikiri tumerudi tukiwa wachangamfu sana. Ninataka kumshukuru Rais kwa Hotuba yake madhubuti ambayo alitoa jana hapa katika hili Bunge. Kwanza, aliyakariri yale mambo yote ambayo Serikali hii imefanya, akikumbuka kwamba hiki ndicho kikao cha mwisho cha Bunge la Tisa kabla uchaguzi kufanywa. Ilikuwa ni jukumu lake kukariri huduma ambazo Serikali yake imetoa katika kipindi cha miaka mitano ambacho kitakwisha mwezi wa Disemba. March 21, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 15 Kwanza, alitaja habari ya elimu na sote tunaweza kukubaliana kwamba sera ya elimu katika nchi yetu hii imefaulu sana. Alipozindua elimu ya msingi bila malipo, kulikuwa na watoto wachache sana katika shule za msingi. Baada ya kuzindua sera ya elimu bila malipo, ni watoto zaidi ya milioni mbili ambao walijiunga na shule za msingi. Sasa ni watoto karibu milioni nane walioko katika shule za msingi. Vile vile, katika sera ya elimu, Serikali imefanya watoto wakawa wengi katika shule za upili. Wakati huu tuna watoto karibu laki nane ambao wamejiunga na shule za upili. Rais alitaja jambo la kuimarisha matibabu katika nchi hii yetu. Hapo awali Mkenya alipokwenda kwenye dispensari alikuwa anaitishwa karatasi ili waweze kuandika matakwa yake ambayo atapeleka mahali pa kununua hizo dawa. Sasa ukienda hata huko mashinani utakuta kuwa kuna dawa za kutosha. Hata katika hospitali nyingine kuna dawa za kupigana na virusi vya Ukimwi. Bw. Spika, Rais vile vile alitaja huduma ambazo zinapelekwa katika sehemu ambazo zinakabiliwa na ukame kama kule Mandera na kwingineko ambapo tumejaribu sana kuchimba mabwawa na kusambaza maji katika sehemu mbali mbali. Wakati ukame ulipokuwa umezidi hata Serikali ilianza kunua majani na kuyapeleka katika sehemu hizo ili ng'ombe wa hao watu wapate chakula kama wanadamu. Barabara ambazo zilikuwa zimeharibika katika Jamuhuri yote zimeanza kurekebishwa. Kokote unakoenda utakuta kuna mashine ambazo zinafanya kazi; sio tu kurekebisha na kukarabati zile barabara za zamani, bali kufungua barabara nyingine mpya. Kuna wakati ambapo kulikuwa na mafuriko na barabara na daraja zikaharabika lakini Serikali iliona kwamba watu waliokuwa wamezingirwa na maji wameokolewa. Barabara na daraja ambazo zilikuwa zimeharibika zimetengenezwa. Wakati wa baa la njaa, kuna chakula kingi ambacho kilipelekwa kwa wananchi. Hatukununua chakula hicho kutoka ng'ambo kama ilivyokuwa siku za zamani. Tulitumia pesa zetu kununua mahindi kutoka kwa wakulima wetu nao wakafanikiwa kwa kupata pesa hizo. Tumefufua uchumi. Sasa uchumi unaanza kukua kwa kiwango cha asilimia sita na hii ni kwa sababu ya muongozo wa Serikali hii ambao umetilia maanani kuona kwamba wametengeneza mazingira bora ambayo yataweza kuwasaidia wenye kuleta rasilmali katika nchi hii. Lakini zaidi tulikuwa tunaangalia wale wananchi wa Kenya ambao wenyewe walianza---"
}