GET /api/v0.1/hansard/entries/229601/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229601,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229601/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Awori",
"speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
"speaker": {
"id": 290,
"legal_name": "Moody Arthur Awori",
"slug": "moody-awori"
},
"content": " Bw. Spika, nilikuwa nikisema kwamba uchumi wetu umeboreshwa kwa sababu ya muongozo mwema wa Serikali hii na imeweka mazingara bora ambayo yamewawezesha wananchi wetu kuweka pesa katika biashara hapa. Sasa wanaendelea kufanya hivyo. La muhimu ni kwamba Rais alionyesha dhamira yetu ni nini; ni matakwa gani tuliyonayo na tutaweza kuyatimiza namna gani. Licha ya changamoto nyingi ambazo zinakumba nchi yetu, kuna mipango mingi sana ambayo imefanywa iliyowezesha uchumi wetu kuendelea mbele. Kwa mfano, wakati tulipounda Serikali hii, tulisema kuwa kutakuwa na nafasi nyingi za ajira ya kutosha watu wetu lakini wengi wa wale ambao hawaungi mkono Serikali wanauliza hiyo ajira iko wapi. Jambo hili lilifanya Serikali kuanzisha hazina ya vijana kwa sababu tunajua katika nchi yetu, idadi kubwa ni ya vijana. 16 PARLIAMENTARY DEBATES March 21, 2007 Kiwango cha 73 kwa 100 ni vijana ambao wako chini ya umri wa miaka 30. Ikawa sasa ni muhimu tuangalie \"informal sector\" ili tujaribu kuwasaidia vijana wetu waweze kujitegemea wenyewe. Kukawa na hazina ya vijana ambayo kazi yake ya kwanza ni kuwafunza vijana jinsi ya kuendesha biashara ndogo ndogo. Ya pili ni kuwapa mikopo ambayo itawawezesha kuendesha hizo biashara. Hiyo hazina itawasaidia sio tu kuwafunza jinsi ya kuendesha biashara, bali jinsi wanaweza kukopa, kununua bidhaa ambazo watatengeneza na jinsi ya kuuza hizo bidhaa. Hii imeweza kusaidia kwa sababu ikiwa kijana mmoja anajitolea kujitegemea kufanya biashara ataweza kumuajiri mwenzake. Hii imeongeza ajira kwa vijana. Katiba Hotuba yake, Rais alitaja kwamba hiyo hazina vile vile itaanzishwa kwa upande wa akina mama. Tunajua kuwa ukiangalia maslahi ya mama mboga na wengine, hawa ndio wanaoendesha biashara kubwa sana katika nchi hii lakini wamekumbwa na ukosefu wa kupata mikopo kutoka mabenki makubwa. Ni jambo muhimu sana kuona kwamba sasa kutakuwa na hazina ambayo itawasaidia akina mama kupata mikopo. Pia watafundishwa jinsi wanaweza kuendesha biashara ili kwa mfano, wakianza biashara na shilingi laki moja baada ya miaka miwili au mitatu watakuwa na nusu milioni na kadhalika."
}