GET /api/v0.1/hansard/entries/229604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 229604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229604/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Awori",
"speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
"speaker": {
"id": 290,
"legal_name": "Moody Arthur Awori",
"slug": "moody-awori"
},
"content": " Bw. Spika, mbali na kuongeza hazina ya akina mama, Serikali imeimarisha sekta ya utalii na imeenda mbele sana. Wakati tulipochukua usukani watalii chini ya 700,000 ndio waliokuwa wakija katika nchi hii. Mwaka uliopita, watalii wapatao milioni moja na nukta nane walikuja katika nchi hii na wakatumia pesa zaidi ya Kshs6.5 bilioni. Hii sekta inaendelea. Tumeweka maanani jambo hili ili watu waweze kuwa wawekazaji bila kuwafikiria wageni peke yake. Tunataka Wakenya wawe wawekezaji. Tumeona jinsi walivyojifanya wawekezaji katika KenGen, Eveready Battery na kwingineko. Wananchi sasa wanakuja mbele kutoa pesa ambazo walikuwa wameficha kwingineko kwa sababu ya muongozo mwema wa Serikali hii. Bw. Spika, elimu ya upili ni jambo lingine ambalo mhe. Rais ametaja kwa kusema kwamba Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu na wengine watakuja kukaa pamoja ili waangalie swala hili. Labda haitakuwa elimu ya upili bila malipo, lakini itarahisishwa kidogo ili wananchi waweze kuwapeleka watoto wao katika shule za upili. Pia, mhe. Rais alitaja katika Hotuba yake kwamba, labda itakuwa jambo la busara iwapo Wabunge watafikiria habari ya ujenzi wa shule za upili ambazo watoto watasoma mchana na kurudi nyumbani. Hiyo inaweza kuwa rahisi kidogo kwa wale ambao hawajiwezi kwa njia zingine. Bw. Spika, mhe. Rais pia alitaja kwamba watakuja kuongeza usaidizi katika sehemu kame au Arid and Semi-Arid Lands (ASALs) na watakuja kuweka mkazo vile vile, kwa kuwapatia maji na kuleta nguvu za umeme katika sehemu kama hizo. Huu ndio mwelekeo wa Serikali hii, ambayo kazi yake itafanywa mwaka huu. Tunajua kwamba kuna mipango ya kusambaza nguvu za umeme katika kila sehemu ya nchi hii. Wakati huu, kuna miradi 930 ya kueneza nguvu za umeme kwa sababu tunajua kwamba nguvu za umeme husaidia ile sekta ya Jua Kali. Sasa, vijana wataweza kutengeza vifaa kwa njia ya urahisi. Na sio hiyo peke yake; nguvu za umeme zinasaidia shule kwa kuwa na kompyuta zinazowawezesha kuwasiliana na wengine kwa njia ya mtandao. Bw. Spika, mhe. Rais pia alitaja habari ya kilimo. Tunaona kuwa wale wanaolima pareto, March 21, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 17 kahawa na majani chai watakuja kusaidiwa, ili waweze kuongeza kilimo chao. Pia, wale wanaouza watatakikana kuongeza thamani kwa hizo bidhaa; valueaddition ni jambo ambalo alilotaja na ndio mwelekeo mpya ambao tunautaka. Vile vile, mhe. Rais ametaja habari ya kuimarisha uvuvi. Serikali hii imeweka nguvu za umeme kando ya Ziwa Victoria, ambako kumewekwa viwanda vya kutengeza barafu ili waweze kuhifadhi samaki ndio waweze kupata bei nafuu kwa sababu, siku zilizopita, wale wachuuzi walikuwa wanawadanganya wavuvi kwa sababu ukosefu wa barafu uliwafanya wauze samaki kwa haraka. Mhe. Rais pia hakuwasahau wafanyabiashara wadogo wadogo, tunaowaita hawkers . Bw. Spika, hivi majuzi, wameanza kujenga soko kubwa kule Muthurwa ambako hao wafanyabiashara wadogo wadogo wataweza kujipatia riziki yao huko. Huo ni mwanzo tu na pia tutakwenda kufanya hivyo huko Mombasa, Nakuru, Kisumu na kwengineko ili wale watu wadogowadogo nao wapate riziki zao. Tumeimarisha uhusiano kati ya Serikali na sekta ya kibinafsi kwa sababu uchumi hauwezi kuimarika ikiwa hakuna uhusiano na urafiki mwema kati ya Serikali na sekta ya kibinafsi. Hii imefanya wale walioko katika sekta ya kibinafsi kuchukua jukumu la kuwasaidia wananchi kwa mipango fulani-fulani. Sasa, tunaona makampuni makubwa yanaanza kuwasaidia watoto wetu kwa"
}