GET /api/v0.1/hansard/entries/229608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 229608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/229608/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Awori",
    "speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
    "speaker": {
        "id": 290,
        "legal_name": "Moody Arthur Awori",
        "slug": "moody-awori"
    },
    "content": ". Mhe. Rais pia alitaja habari ya kupigana na ufisadi, na hili ni jambo ambalo Serikali inaendelea nalo, hata akasema kwamba sasa wataleta Mswada ambao utafanya watu kuonyesha mali walionayo, jinsi walioipata na ilikuwa namna gani. Bw. Spika, kurekebisha Katiba ni jambo ambalo limezungumzwa na kila mtu na kadhalika. Watu wengi walimuuliza Rais kuchukua muongozo, na yeye amechukua muongozo akasema sasa tuanze kuzungumza na tujadiliane, ili tuweze kutatua jambo hili kwa sababu Katiba ni jambo la watu wote. Sio jambo la Mbunge au diwani, bali ni jambo la kusaidia nchi hii yote. Lile linalotakikana ni kwamba wakati tunazungumza, tusiwe tunaangalia hii Katiba itanifanyia mimi nini kibinafsi, bali tuangalie hii Katiba itakuja kusaidia nchi yetu na vizazi vyetu vinavyokuja kwa namna gani. Siku ya Jumatatu ya wiki inayokuja tutaanzisha mazungumzo ili tuweze kuona tutafika wapi. Mwisho, Bw. Spika, mhe. Rais ametaja na kusema kuwa kutakuwa na Miswada mingi ambayo italetwa hapa ili iweze kutoa miongozo ya sekta fulani. Kwa mfano, wakati huu tuko na uhaba wa Mahakimu, na mhe. Rais amesema kwamba kutakuwa na Mswada ambao utampa mamlaka ya kuongeza Mahakimu kutoka 60 hadi kufikia 200. Hili ni jambo tunalolingojea. Pia, kutakuwa na Mswada kuhusu vyama vya kisiasa ili tuweze kuona vyama vya kisiasa vinaendelea namna gani. Nikimaliza, napenda kusema kwamba sote yafaa tuunge mkono na tumshukuru Rais, ijapokuwa mtu akiwa katika upande wa Upinzani, kazi yake ni kukosoa na kadhalika. Lakini ikiwa kuna mambo ambayo yako sawa, tuseme mambo yako sawa na Rais huyu amefanya jambo muhimu; ameonyesha njia."
}