GET /api/v0.1/hansard/entries/230106/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 230106,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/230106/?format=api",
"text_counter": 363,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Karume",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 234,
"legal_name": "Njenga Karume",
"slug": "njenga-karume"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nitoe maoni yangu kuhusu Hoja hii. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuwakumbusha waheshimiwa Wabunge ambao hawataki tuende nyumbani leo kwamba tuko na kazi hapa Bungeni, na pia katika maeneo yetu ya uwakilisha Bungeni. Hii ndio sababu tumekuwa tukienda likizo mara kwa mara. Kwa miaka yote ambayo nimekuwa katika Bunge hili, tumeenda likizo, na naona kuwa wakati huu ndio unaofaa kwa sababu kuna kazi nyingi sana huko nje. Wakati huu, mvua imenyesha sana na imeharibu shule nyingi na mito mingi imefurika. Huu ndio wakati mzuri wa kwenda likizo ili tuwe na watu wetu waliotuchagua kwa sababu wameathiriwa na mvua. Kwa hivyo, ni muhimu sana twende likizo sasa ili tukawasaidie watu wetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, Serikali hii imeleta maendeleo mengi sana nchini. Kwa mfano, Serikali imeanzisha hazina ya maendeleo katika sehemu za uwakilishi Bungeni, yaani, Constituencies Development Fund (CDF). Kwa hivyo, wakati huu ambapo shule zimefungwa inafaa tuende likizoni ili tuweze kupanga miradi ya CDF. Najua wale wanaoipinga Hoja hii wanataka tuendelee kufanya kazi hapa Bungeni. Hata hivyo, kazi inayotungojea katika sehemu zetu za uwakilishi Bungeni ni nyingi sana. Natoa pongezi kwa Serikali hii inayoongozwa na Rais Mwai Kibaki kwa kuimarisha mambo mengi kama vile uchumi. Hali ya barabara zetu ilikuwa mbaya sana kabla ya Serikali hii kuchukua uongozi. Lakini wakati huu wilaya nyingi zina barabara za lami. Kwa hivyo, tunafaa kuipongeza kazi inayofanywa na Serikali hii. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii ili tuende likizoni. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna vitu kadhaa ambavyo tunafaa kuvilinda, kwa mfano, Ikulu yetu. Wakati tunapoongea, tunafaa kujua kwamba Ikulu ndio roho yetu katika nchi hii. Kuna watu wanaosema kwamba wataandamana hadi Ikulu ya Nairobi. Hatujawahi kuona mambo kama hayo. Wengi wetu tulikuwa katika Upinzani kwa zaidi ya miaka kumi, wakati Rais Mstaafu, Bw. Moi, alikuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Hatukuwahi kuzungumza juu ya mambo kama hayo. Hata tukikasirika hatufai kufikiria mambo kama hayo. Tukienda likizoni, tunafaa tusahau tofauti 4300 PARLIAMENTARY DEBATES December 7, 2006 zetu hapa Bungeni. Tunafaa kuzungumza pamoja ili tutatue tofauti zetu. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}