GET /api/v0.1/hansard/entries/230179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 230179,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/230179/?format=api",
"text_counter": 436,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Moroto",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Health",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia Hoja hii. Ni wakati ambapo sisi Wabunge tunatarajia kwenda kukutana na watu wetu na kukagua miradi ambayo tumekuwa tukifanya kwa muda mrefu. Ningependa kuishukuru hii Serikali kwa yale yote ambayo imefanya kwa miaka minne ambayo imekuwa uongozini. Tukiyalinganisha maendeleo yaliyoletwa na Serikali hii kwa miaka minne na kazi ya Serikali iliyopita ambayo ilikuwa uongozini kwa miaka 40, tutatambua kwamba Serikali hii imewafikishia maendeleo hata wale watu ambao walikuwa wamesahaulika kwa muda mrefu. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakilisho langu liko katika eneo linalojulikana sana katika historia ya Kenya. Mashujaa waliopigania Uhuru wetu walifungwa huko. Ajabu ni kwamba walipoachiliwa, walisahau sehemu hiyo na maendeleo huko yakabaki nyuma. Hata hivyo, ukizuru 4308 PARLIAMENTARY DEBATES December 7, 2006 wakilisho langu leo, utaona kwamba kuna mambo yanafanyika. Watu angalau wanapatiwa madawa na kuna stima. Kitambo, watu wengi huko kwetu hawakujua stima ni nini. Hata watoto shuleni wakiulizwa waeleze stima ni nini wao hujibu eti ni waya. Hii leo tunaweza kusema kuwa kuna maendeleo kule kwetu. Hili ni jambo linalotupa moyo kwa sababu miradi ya Serikali hii impenyeza kila sehemu ya nchi hii. Serikali iliyopita ilikuwa inawachunguza Wabunge wenye siasa kali na kuwanyima maendeleo kwao. Wakati huu mambo ni tofauti kwa sababu hata Wabunge wa Upinzani wanaweza kushuhudia kwamba hawajabaguliwa na Serikali hii. Maendeleo yamesambazwa kila sehemu ya nchi. Hilo jambo limetupatia moyo kabisa. Kuhusu usalama, wengine wetu hapa ndio tunajua maswala ya usalama yanapotajwa. Wakati wa Serikali iliyopita jambo kidogo la kutishia usalama lingetendeka, majeshi pamoja na ndege za kivita yalikuwa yakimwagwa mahali kwenda kutatiza maisha ya watu. Tendo hili halikusuluhisha matatizo ya watu. Kazi ya majeshi hayo ilikuwa ni kuwapiga watu tu na kuvuruga usalama. Baada ya kumaliza shughuli yao, wao walilipwa hela na kuondoka huku wakiwaachia wananchi mateso matupu. Wakati huu, majeshi yanayotumwa kulinda amani hayasumbuwi watu. Ukweli ni kwamba majeshi hayo yanajishughulisha na miradi ya kuwafaidisha wananchi. Ningependa kumshukuru Waziri anyehusika na mambo ya usalama kwa tendo hilo. Aidha, ningependa kumshukuru Rais wa nchi hii kwa vile yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yetu."
}