HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 231252,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231252/?format=api",
"text_counter": 647,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Spika, shukrani kwa kunipa nafasi na mimi nichangie angaa kwa kidogo tu Ripoti hii ya Kamati ya Bunge inayosimamia matumizi ya pesa za Serikali. December 6, 2006 PARLIAMEANTARY DEBATES 4265 Bw. Spika, sitaki kurudia yale ambayo nilisema jana isipokuwa kusisitiza kwamba haifai yale mambo ambayo huwa yamemulikwa katika ripoti zilizopita yanaendelea kumulikwa katika Ripoti hii mpya. Hiyo ni ishara ya kwamba matatizo huwa hayatatuliwi bali yanaendelea kuweko pamoja na kazi yote ile ambayo Bunge huwa inafanya katika juhudi za kumalizia nchi yetu matatizo ya ufisadi. Bw. Spika, niongezee ya kwamba wakati tulikuwa tunazunguka nchi hasa tukikagua miradi ya barabara, lilikuwa ni jambo la kushangaza kuona idadi ya pesa zinazopotea kupitia miradi ile kwa sababu kanuni za ujenzi hazifuatwi vilivyo. Tulikuta barabara imejengwa mwaka huu na baada ya miaka miwili, barabara hiyo inakuwa imejaa mashimo. Tukauliza: \"Inakuwaje barabara haiwezi kumaliza hata miaka mitatu wakati tunajua ya kwamba kuna barabara kama ile ambayo ilijengwa na mateka wa Italiano mwakani 1945 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na barabara hiyo ilikuja kubambuka majuzi tu miakani ya sabini ama themanini? Hiyo ni barabara ambayo imekaa zaidi ya miaka thelathini ikiwa pale katika hali ya uzima. Lakini barabara za leo, unakuta inajengwa baada ya miaka miwili imebambuka na inataka kujazwa mashimo au inataka kuondolewa kabisa ijengwe upya. Bw. Spika, lilikuwa ni jambo la kushangaza tulipokuwa tunawauliza wahandisi wa barabara: \"Barabara ya kawaida inatakiwa ikae miaka mingapi\"? Wahandisi walituambia: \"Sisi hatuna habari\". Tukawauliza: \"Sasa kama muhandisi hana habari barabara inatakiwa ikae miaka mingapi ndio iharibike, nani atakuwa na habari?\" Unakuta barabara zinajengwa kwa kutumia ufisadi wa hali ya juu. Wakati mwingine, unakuta barabara ambayo inatakiwa iwe na ukubwa wa lami tuseme inchi kama nne, badala yake inawekewa ukubwa wa nchi mbili na pamoja na kupunguzwa kwa ukubwa wa lami, malipo yanakuwa ni yale yale. Unakuta nchi imeingia hasara kubwa. Mabilioni ya shilingi yamepotea kupitia ufisadi wa aina ile. Bw. Spika, jambo la kushangaza zaidi ni kwamba wahandisi wanaohusika na ufisadi huo wanaendelea kuwemo kazini mwaka baada ya mwingine, mpaka wanastaafu. Watu wanafanya kazi kinyume na kanuni zilizopo na kujipatia pesa kupitia ufisadi. Ijapokuwa jana ulisema kwamba ufisadi ambao haujathibitishwa na mahakama hauwezi kuitwa ufisadi, kama watu fulani wanaweza kusababisha nchi hii kupata hasara kubwa kiasi hiki halafu waendelee kuhudumu katika nyadhifa zao mpaka wastaafu uzeeni, ni lazima kuwe kuna kasoro kubwa; kasoro ambayo inahitaji kurekebishwa, kwa sababu nchi hii haiwezi kuendelea bila ya kuwepo kwa barabara na miundo msingi mingine inayohitajika. Ni lazima tuzijenge barabara zetu vizuri na kuiokoa nchi hii kutokana na hasara inayosababishwa na utendakazi duni na hasara inayosababishwa na kutofanya vyema kwa uchumi. Tulitembelea sehemu za Eldoret, Ziwa Victoria na Chepterit ili tujionee hali ya barabara. Tulipata kwamba, gharama ya ujenzi wa barabara katika sehemu hizo tayari ilikuwa imeshalipwa lakini hakuna barabara iliyokuwa imejengwa. Ni jambo la kushangaza kwamba barabara zilikuwa zimelipiwa gharama zote za ujenzi lakini barabara hizo hazikuepo. Unashindwa kufahamu haya ni mambo ya aina gani. Hata unashindwa useme nini. Hata ni afadhali ile barabara inayojengwa kiholela na kupata mashimo baada ya miezi kadhaa kuliko barabara ambayo haipo, licha ya kwamba gharama ya ujenzi wake imelipwa, na hakuna mtu wa kuadhibiwa. Wakati mwingine unajua kwamba, kweli, tuko na shida. Bw. Spika, sasa ningependa kuzungumzia suala la ofisi ya Mkuu wa Sheria. Kazi iliyofanywa na ofisi hiyo imeiletea nchi hii hasara isiyo na kifani. Serikali imepoteza mabilioni ya pesa wakati wa enzi ya Rais mstaafu, Daniel arap Moi, na wakati wa enzi ya Rais Kibaki, kwa sababu ya ushauri mubaya kutoka kwa Ofisi ya Mkuu wa Sheria. Bw. Spika, wakati mmoja, tulipotembelewa na Mkuu wa Sheria, tulimtaka atueleze ni kwa nini ofisi yake haitoi ushauri muafaka kwa Serikali wakati wa kuandika mikataba. Pia, tulimtaka 4266 PARLIAMENTARY DEBATES December 6, 2006 atueleze ni kwa nini ofisi yake haitumii mawakili kortini kuiwakilisha Serikali pale Serikali au Wizara ya Serikali inaposhtakiwa, na kwa hivyo basi kusababisha Serikali kupoteza kesi na kulazimika kulipa kiasi kikubwa cha pesa kama fidia kwa mlalamishi. Kwa sababu ya hasara kubwa iliyopatikana, tulimshauri Mkuu wa Sheria afikirie kujiuzulu ili kuteuliwe mtu mwingine ambaye atafanya kazi bora kuliko yeye. Sijawahi kuona mtu mkali kama alivyokua Mkuu wa Sheria siku hiyo. Aliwaka kama moto, na inaeleweka. Hakuna mtu ambaye anataka kuacha kazi. Lakini, ni lazima kila mtu afanye kazi kwa namna inayoleta faida, na siyo kwa namna inayoleta hasara mwaka baada ya mwingine. Bw. Spika, kazi ya Mkuu wa Sheria ni kuisaidia Serikali isipate hasara kutokana na maswala ya kisheria. Kama Serikali inapata hasara, mwaka baada ya mwingine, kupitia njia hiyo, licha ya kuwepo kwa Mkuu wa Sheria aliyefuzu vyema katika maswala ya kisheria, ni lazima ieleweke kwamba kuna kasoro ya utendakazi katika ofisi hiyo. Ni vigumu kujua jinsi ya kuirekebisha kasoro hiyo. Ni kwa kum---"
}