GET /api/v0.1/hansard/entries/231308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 231308,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231308/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninafikiri kwamba anajibu maswali ya ulimwengu uliopita. Waziri Msaidizi hawezi kusema kwamba daraja liko chini ya mto na mto unapofurika unafagia wale waliomo. Waziri Msaidizi hajui kwamba kutoka Kapenguria hadi Turkana kuna daraja ambazo ziko chini, na mto unapofurika hata dereva hawezi kujua kiwango cha maji? Je, Wizara ya Barabara na Ujenzi itarekebisha madaraja yaliyojengwa na wakoloni lini?"
}