HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 231546,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231546/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Spika, nilikuwa nakutolea shukrani zangu kwa kunipa fursa hii ili nitoe mchango wangu juu ya Ripoti ya Kamati inayosimamia matumizi ya pesa za Serikali. Bw. Spika, uchunguzi dhidi ya ufisadi ni muhimu sana. Hakuna nchi ambayo inaweza kuendelea ikiwa ina tatizo la ufisadi. Ni lazima tukubali ya kwamba ufisadi ni tatizo kubwa katika nchi yetu. Shirika la Transparency International, katika ripoti yake kila mwaka huonyesha ya kwamba ufisadi unaendelea kukithiri hapa nchini. Ripoti hiyo inaungwa mkono na Ripoti hii ya Kamati ya Bunge. Hatuwezi, kwa upande mmoja, kusema tunataka kupiga vita umaskini ikiwa kwa upande wa pili tunaruhusu ufisadi kukithiri hapa nchini. Ni lazima tuupige ufisadi vita kwa sababu una mazoea ya kuenea. Nadhani kila aina ya ushahidi unaonyesha ya kwamba ufisadi umezidi badala ya kupungua hapa nchini. Wengi wanasema ya kwamba ufisadi umezidi kwa sababu idadi ya watu katika nchi hii inaongezeka kwa kasi sana. Hiyo si sababu tosha ya ufisadi kuendelea. Bw. Spika, utakumbuka tulipotembelea nchi ya Uchina, Meya wa jiji la Shangai alikuwa ametiwa mbaroni siku chache kabla ya sisi kuingia mji huo kwa madai ya ufisadi. Meya huyo ni mtu mwenye cheo kikubwa katika mpangilio wa Serikali ya Uchina na ana mamlaka makuu katika chama kinachotawala. Lakini hata hivyo, alitiwa nguvuni kwa madai ya ufisadi. Labda ataokolewa ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha. Kulingana na kiasi cha pesa anachotuhumiwa kuchukua anaweza kunyongwa. Nadhani ni hatua za aina hiyo peke yake ambazo zinaweza kutusaidia kupunguza ufisadi nchini. Bw. Spika, nilikuwa mwanachama wa Kamati hii kabla ya kuteuliwa kama Waziri Msaidizi. Ninakumbuka ya kwamba katika vikao vyetu tulikuwa na tatizo kubwa tukitafuta ukweli kutoka kwa maofisa fulani wa Serikali. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba wakati maofisa wa Serikali wanakutana na wanachama wa Kamati hii, ni kana kwamba wamo vitani. Wanachama wa Kamati hii kila mara hutafuta ukweli wa mambo lakini maofisa hufanya kila jitihada kuuficha ukweli huo. Nilikuwa ninajiuliza: Kwa nini tusiwe na lengo moja kama wanakamati na maofisa wa Serikali? Ni wajibu wa maofisa wa Serikali kusaidia Kamati kupata ushahidi ambao utaisaidia Serikali kukomesha ufisadi. Haiwezekani ya kwamba maofisa wa Serikali wanachukua hatua ya kuficha ukweli wa mambo. Tulisukumana na maofisa na wakati mwingine kutoa vitisho ili tupate habari wanazozijua. Sijui ni hatua gani itakayochukuliwa ili maofisa wa Serikali wajue ni jukumu lao la kupigana na ufisadi hapa nchini. Sijui ni hatua gani nyingine inaweza kuchukuliwa ili kuhakikisha ya kwamba hawafanyi mchezo wa kuficha ukweli wanapoulizwa maswali na wanachama wa Kamati. Bw. Spika, tatizo lingine ni lile la Kamati hii kutoa mapendekezo ya kupigana na ufisadi Serikalini na pia katika mashirika, lakini hayatekelezwi. Ukisoma Ripoti hii, utaona mapendekezo yaliyomo ni yale yaliyokuwemo katika Ripoti ya mwaka uliotangulia. Hata Ripoti ya mwaka uliofuata huu, itakuwa na mapendekezo haya haya. Je, kuna haja gani kutoa mapendekezo ambayo hayatekelezwi? Pia inatatiza ya kwamba wakati huu, Waziri anayehusika hayuko hapa Bungeni. 4138 PARLIAMENTARY DEBATES December 5, 2006 Ingekuwa vizuri kama angekuwepo ili asikie Bunge likijadili mambo haya. Pia ingekuwa vizuri ikiwa maofisa wa Wizara yake wangekuwa hapa kwa sababu Ripoti hii imechukuwa muda mwingi wa waheshimiwa Wabunge kuitayarisha na kuijadili. Kama hakuna hatua itakayochukuliwa, hakuna haja ya kuwa na Kamati hii na kuja na Ripoti kama hii ambayo tunaijadili hapa Bungeni ikiwa haitatekelezwa. Hili ni jambo ambalo linatia hofu, ya kwamba ukiwa mwanachama wa Kamati hii, matatizo mliyoyajadili miaka miwili iliyopita, mnaendelea kuyajadili hata wakati huo. Unashindwa kama hakuna mtu ambaye anatakiwa ahakikishe ya kwamba tatizo lililojadiliwa mwaka jana halitajadiliwa mwaka huu kwa sababu litakuwa limetatuliwa. Na lile ambalo linajadiliwa mwaka huu halitajadiliwa mwaka ujao kwa sababu litakuwa limetatuliwa. Huu umekuwa mchezo wa kupoteza wakati kwa sababu matatizo na mapendekezo ni yale, yale, lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Hili ni jambo la kuvunja moyo na ambalo halifai kuwepo. Sijui Bunge linaweza kujipatia uwezo gani ili kuuliza Wizara husika kutekeleza mapendekezo haya. Sijui kama ni Wizara ya Fedha ambayo ina wajibu wa kuteleza mapendekezo haya. Ni lazima kupatikane namna ya Bunge kushinikiza Wizara inayohusika ili itekeleze mapendekezo haya la sivyo tutakuwa tunapoteza wakati na pesa nyingi za nchi hii tukijadili matatizo ambayo yanastahili kuondelewa moja kwa moja. Matatizo haya yasipoteuliwa, nchi itaendelea kutatizika na wananchi wataendelea kuumia. Bw. Spika, jambo lingine ambalo ningependa kugusia ni lile la kuwasilisha Ripoti hii kwa tume ya kuchunguza na kupigana na ufisadi inayojulikana kwa umaarufu kama Kenya Anti- Corruption Commission (KACC). Ningependekeza ya kwamba hata wakati Kamati ya Bunge inapokutana, iwe na mwakilishi kutoka tume ya KACC na idara ya upelelezi ya polisi. Ikiwa kumesemwa jambo ambalo lina dhihirisha ya kwamba pamefanyika uhalifu, sheria imevunjwa au ufisadi umefanyika, hakuna haja ya kungojea, kwa maoni yangu, mpaka Ripoti hii ijadiliwe hapa Bungeni kabla ya hatua kuchukuliwa. Kama mtu amehusika na ufisadi, inafaa achukuliwe hatua na polisi wakati anapohojiwa. Haifai kwetu kungojea hadi mtu afe kabla hajachukuliwa hatua? Mara nyingi hizi ripoti ni kama postmortem . Kama inawezekana ufisadi uzuilike, ni afadhali kuzuia kuliko kutibu. Hili ni pendekezo lililotolewa na Kamati na sijui litatekelezwa vipi. Wale ambao wanapigana na ufisadi kutoka idara zingine za Serikali wanafaa kushirikiana na Kamati hii ya Bunge katika kupigana na ufisadi kwa sababu adui ni mmoja na kuna faida kubwa ya kushirikiana kuliko kila idara kupigana kivyake bila ya kusaidiana. Bw. Spika, hata kama hakuna ofisa wa KACC katika vikao vya Kamati ya Bunge, ingekuwa ni bora sana kama tume hii inaweza kuchukua ripoti hizi na kuzifanyia uchunguzi wa kina kuona kama zina msingi. Hii ni kwa sababu ripoti hizi kwa jumla zinaongea juu ya wizi. Lakini ukizisoma, utaona kwamba lugha inayotumiwa sio ya moja kwa moja. Haitaji neno \"wizi\" au \"ufisadi\". Ni lugha nyingine ya kuficha mambo. Kwa mfano, utasikia mtu alichukua pesa, lakini badala ya kusema aliiba pesa za Serikali, lugha ya Ripoti hii, na ndio inatumika katika Kamati, inakuwa ni lugha ya \"Ofisa alijikopesha pesa.\" Kujikopesha pesa za Serikali ni kuiba. Lakini, inaposemekana kwamba alijikopesha---"
}