GET /api/v0.1/hansard/entries/231548/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 231548,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231548/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Hiyo ni kweli kabisa, Bw. Spika. Lakini jambo ninalosema ni kwamba, haya tukubali ya kwamba Kamati hii haiwezi kuongea juu ya wizi au ufisadi wa moja kwa moja kwa sababu haujathibitishwa mahakamani. Basi ni muhimu baada ya kuonekana mtu amejikopesha pesa asukumwe mbele ili kuonekane kama kulikuwa wizi au la. Lakini ikibaki tu kwa ripoti kwamba mtu alijikopesha pesa, itabaki hivyo hivyo bila kufuatiliwa. Utakuta ya kwamba mabilioni ya pesa ambazo zinaongewa juu yake katika hizi ripoti, hakuna mtu ambaye anafuatilia. Bw. Sika, kwa hivyo, kuna haja kubwa ya tume inayochunguza ufisadi, KACC, ichukue December 5, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 4139 ripoti hizi na iende ikazifanyie kazi ili kupunguza ufisadi ambao ninaamini unaendelea sana katika karibu idara zote za Serikali. Mambo haya hayajaisha. Watu bado wana tabia ile ya zamani. Hawajajua kufanya mambo kwa namna nyingine. Ni kama vile Waswahili wanavyosema, \"aliyezoea vya haramu, vya halali hawezi.\" Bw. Spika, jambo lingine ambalo mtu anashawishika kuongea juu yake ni lile la wale ambao wamejitwika jukumu la kukosoa Serikali kwa ufisadi. Ni kama kwamba wao hawawezi kupatikana katika jambo lile. Ninaongea juu ya ripoti ambazo zimekuwa zikitolewa na shirika la Transparency International; shirika ambalo linafanya kazi nzuri. Lakini wakati mwingine, unashindwa wale ambao wamejitwika jukumu hilo la kumulika wengine wao huwa wanamulikwa na nani? Mwanzoni mwa mwaka huu, kulikuwa na tatizo la wakurugenzi wa shirika hili kushtakiana ya kwamba wengine wamehusika na visa vya ufisadi. Tulisikia ya kwamba Kamati iliundwa ya kuchunguza jambo hilo. Ripoti ya Kamati hiyo bado hatujaipata na hatujui kama ilifanya kazi au la. Lakini sidhani kuwa kunaweza kuwa na aina tofauti za ufisadi; kwamba kuna watu ambao wanaweza kufanya ufisadi na ufisadi huo usionekane kama ufisadi lakini wengine wakifanya, ufisadi wao unamulikwa zaidi. Ningetaka hili shirika linalo kuambia ni nani mfisadi na ni nani si mfisadi lituongoze kwa mfano. Kama imesemekana wenyewe wameshtakiana hadharani na kamati imeundwa ya kuchunguza ufisadi uliyomo katika shirika hili, basi nchi ina haki ya kupewa matokeo ya uchunguzi huo ili tujue kama kulikuweko na ufisadi au la. Hii ni kwa sababu kama yule anayechunguza ufisadi naye anakuwa mfisadi, hatakuwa na haki tena ya kumulika yeyote. Hatakuwa na haki ya kummulika mhe. Maj. Madoka hapa kwa sababu mwenyewe atakuwa amejifunga."
}