GET /api/v0.1/hansard/entries/231550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 231550,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231550/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": "Kwa hivyo, ni muhimu shirika la Transparency International lituambie uchunguzi wao ulifika wapi. Ni Bw. Mwalimu Mati ambaye alikuwa na makosa au ni mkurugenzi mwenzake, Mungai? Ni nani alikuwa amefanya ufisadi? Tunangojea na hatutaki jambo hili lisahaulike. Wengine ambao wako na jukumu la kujimulika ni watu wa habari. Wanahabari ni watu ambao wako na jukumu kubwa la kumulika ufisadi. Na mara nyingi nimejiuliza kwamba wanapomulika ufisadi wa mhe. Wamwere au mhe. Maj. Madoka, nani huwa anamulika ufisadi wao? Kukifanyika ufisadi kule kwao, hawawezi kutangaza. Ni lazima namna ya kumulika kila mtu itafutwe. Hatuwezi kuwa na wanahabari ambao ni kama wako juu ya sheria ama umulikaji. Sidhani hapa kuna mtu ambaye atakubali kutetea wanahabari kwamba ni watakatifu. Mara nyingi tumekwenda mikutanoni kule, tunamaliza mkutano halafu inakuwa ni kwenda \"chamber\"; ni kusimama kando kabla ya shughuli kuisha. Na usipokwenda \"chamber\" unatandikwa kwa sababu maneno yote ambayo umesema hutayapata kwenye runinga ama gazeti siku ijayo. Huo si ufisadi? Nani anamulika watu hawa wanaotumulika sisi? Kuna wale waandishi ambao wanatoka mashinani. Wanatuma habari zao kwenye vyombo vya habari na watu hawa wanalipwa pesa kidogo sana. Waandishi hao wa habari huambiwa eti hawawezi kupewa Kshs600 ama Kshs700 ambazo wamefanyia kazi kwa mwezi mzima. Kumbuka wanaambiwa hivyo na watu ambao wamekuwa wakipata faida ya mabilioni ya pesa. Kwa mfano, kampuni ya Nation imepata faida ya Kshs1 bilioni mwaka huu. Je, kampuni kama hii itashindwaje kuwalipa wafanyakazi wake walioko kule mashinani? Ikiwa wanashindwa kuwalipa wafanyakazi wake, je, si huo ni ufisadi? Ni nani atamulika ufisadi wa aina hii? Kwa hivyo, vyombo vya habari, kwa njia fulani, vimejipatia 4140 PARLIAMENTARY DEBATES December 5, 2006 mamlaka yakutumulika sisi. Ni lazima viwe tayari kujimulika vyenyewe la sivyo kutafutwe watu wengine ambao wataweza kuvimulika kwa sababu hakuna sehemu ya jamii yetu ambayo haijahusika na tatizo hili la ufisadi. Ikiwa kutakuweko na watu ambao watajiweka juu ya wengine, hiyo haitasaidia kumaliza ufisadi bali itasaidia kuufunika tu. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo jingine muhimu ambalo ningependa kutaja hapa ni swala la ufisadi mashinani. Jumapili iliyopita, nilitazama kipindi kimoja katika runinga ya KBC Channel One ambapo wataalamu walikuwa wanahojiwa kuhusu swala hili la ufisadi. Mmoja wa wataalamu hao alikuwa ametoka kwenye Tume ya Kenya Dhidi ya Ufisadi (KACC). Yeye alisema kwamba kila wakati wanapozunguka kuwahoji watu kuhusu tatizo hili la ufisadi, wanapata habari zinazoonyesha, dhahiri shahiri, kwamba ufisadi huko mashinani ni mwingi mno kuliko ule ufisadi wa Anglo Leasing na Goldenberg. Hii ni kwa sababu mamilioni ya watu huko mashinani wamepunjwa kitu kidogo kila mmoja. Ukijumlisha kwa pamoja, utakuta kwamba ufisadi mkubwa umetendeka huko. Jambo la kushangaza ni kwamba ufisadi huo haumulikwi kama unavyomulikwa ufisadi wa kiwango cha Anglo Leasing au Goldenberg. Katika Wakilisho langu kuna visa vingi vya ufisadi wa aina hii. Wakati makampuni yalikuwa yanauzia wananchi hisa ili yapate pesa za kuwanunulia wananchi hao mashamba, ulifika wakati ambapo maofisa wa utawala wa mikoa walijipatia mamlaka mengi sana kiasi cha kwamba wakuu wa wilaya wengine walinyakua makampuni na mashamba katika wakilisho langu na kujipatia ukubwa. Walijiita \"Chairman-General\" . Wengine walikuwa wakali mno; kwa mfano, Mkuu wa Wilaya aliyeitwa Bw. John Anguka. Yeye alikuwa anawambia watu kwamba, \"Mkicheza nami nitaanguka na ninyi.\" Watu wakaogopa \"kuangukwa nao\". Walipoingiwa na hofu ya \"kuangukwa nao\" mali yao yote ilisombwa. Matrekta na mashamba yao yalinyakuliwa na maofisa hawa wa utawala. Ungemkuta ofisa mmoja wa Serikali amejinyakulia mashamba ya watu hamsini na kuwauzia watu wengine. Walionunua hisa na ambao ndio wastahiki wa kweli wa mashamba hayo waliaachwa nje. Haya mashamba yaliyonyakuliwa yalikuwa yauzwe ndiposa faida ipatikane. Hawa wanyakuzi waliweka pesa zote mfukoni na kujipatia madaraka zaidi. Hatimaye waliondoka sehemu hiyo na kuwaacha wananchi wakiwa na matatizo chungu nzima. Mimi ninakumbuka kupitia faili moja ambayo ilionyesha majina ya watu 47 walionyang'anywa mashamba na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, hayati Hezekiah Oyugi. Yeye, Bw. Oyugi, aliandika kwenye hiyo faili kwamba aliagizwa kufanya hivyo na aliyekuwa Rais wa nchi hii mhe. Moi. Swali ninalojiuliza ni: \"Ufisadi wa aina hii utamulikwa lini?\" Ni lini Serikali itakumbuka kwenda mashinani ili kuwasaidia wale wananchi wadogo ambao wanaumia kule? Dhuluma wanayoipata haistahili kuandikwa magazetini eti kwa sababu ni watu wadogo sana."
}