GET /api/v0.1/hansard/entries/231558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 231558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/231558/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, ninakubaliana nawe. Hata hivyo, nilichokuwa ninasema ni kwamba kuna aina mbili za ufisadi. Kuna ufisadi mkubwa na ufisadi mdogo. Hoja yangu hapa ni kwamba ufisadi mdogo umeachiliwa kuendelea bila kuadhibiwa. Wahusika katika ufisadi huu wanaathiri watu wadogo ambao hawana uwezo wa kufanya lolote. Hoja yangu pia ni kwamba haitoshi Serikali kumulika ufisadi mkubwa pekee yake na kuusahau ufisadi mdogo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuhusu matatizo yaliyoko katika wakilisho langu, Wizara ya Ardhi ilikubali kuunda kamati ambayo ilizunguka katika makampuni na mashamba yote ambayo yalinunuliwa na wananchi ambao walikuwa wameungana kuunda makampuni. Kamati hiyo iliwasikiliza watu wakisimulia namna walivyopunjwa hatimiliki pamoja na mashamba yenyewe. Aidha ilielezwa jinsi ambavyo kuna mashamba ambayo yanamilikiwa na watu watatu au wanne kwa pamoja. Jambo la kushangaza ni kwamba wengine wana hatimiliki ilhali wengine hawana. Watu hawa wanaishi katika uoga, kwa mfano, ikiwa umejenga nyumba yako ya mawe, kuna mtu ambaye anashikilia hatimiliki ya shamba lako na anaweza akaja wakati wowote kukuuliza uhamishe nyumba yako kutoka shamba lake. Kuna watu ambao wana stakabadhi za kuonyesha kwamba walinunua hisa lakini hawajapewa title deed . Hiyo kamati ilifanya uchunguzi wake lakini ulipofika wakati wa kutoa mapendekezo, ikatoweka ghafla. Yalikuwa ni makosa makubwa hayo na nimekuwa nikimwomba Waziri anayehusika aiunde hiyo kamati tena ili imalize kazi yake. Hii ni kwa sababu kutoshughulikia ufisadi wa mashinani ni kosa kubwa. Ni sawa na kuwaumiza wananchi wadogo na walala hoi ambao wana sauti dhaifu kuliko wengine wote. Natumai kwamba Waziri wa Ardhi ananisikiliza na atakubali kurudisha kamati hiyo ili imalize kazi yake. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo jingine ambalo ningependa kugusia linahusu pesa zilizoporwa humu nchini na kuwekwa katika mabenki ya nje. Hivi majuzi, ilikuwa ni aibu kuwasikia wazungu wakituuliza, \"Ni kwa nini hamtuombi msaada tuwasaidie kurudisha pesa zenu zilizoporwa?\" Nchi hii inahitaji pesa nyingi na sisi tunakwenda kuomba pesa hizo kutoka kwa wafadhili."
}