GET /api/v0.1/hansard/entries/232045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 232045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/232045/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. M.Y. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kumuomba Waziri ambaye anahusika na mambo ya usalama katika Ofisi ya Rais kutoa habari kamili kuhusu jambo fulani ambalo lilitendeka mnamo tarehe 24 na 25 mwezi huu, ambapo mtu mmoja alienda kuwakodi maofisa wa GSU kutoka Wilaya ya Kwale kuja hadi tarafa ya Voi kule Taita-Taveta ili kutisha na kuua mifugo na kuwanyang'anya wananchi ambao walikuwa wamelikodi shamba linaloitwa Mutunga Ranch. Hawa maofisa wa GSU waliuwa ng'ombe wawili na madume zaidi ya 30 walitoroka kwa sababu ya milio ya risasi ambazo askari walipiga kwenye hiyo boma ambapo, waliwanyang'anya wachungaji dawa za tsetse fly ya thamani ya Kshs300,000 za kutibu hao ng'ombe na kuharibu vyombo vya kupikia. Hilo ni jambo hatari sana kufanywa na maofisa ambao wanatakiwa kulinda amani. Kwa hivyo, ningemuomba Waziri aichunguze hivyo vitendo na kutoa taarifa kueleza vile hayo mambo yalivyofanyika. November 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 4005"
}