HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 232078,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/232078/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Shakombo",
"speaker_title": "The Minister of State for National Heritage",
"speaker": {
"id": 244,
"legal_name": "Rashid Suleiman Shakombo",
"slug": "rashid-shakombo"
},
"content": " Ninakushukuru, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili niunge mkono Hoja hii, ambayo inaliomba Bunge ruhusa ya kuwasilishwa kwa Mswada utakaowezesha kuanzishwa kwa halmashauri ya bandari huru huko Mombasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kusema kweli, mpango huu umechelewa sana. Ungekuwa umetekelezwa zaidi ya miaka kumi iliyopita kwa sababu wataalam wa maswala hayo waliwahi kufanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti na mapendekezo yao kwa Serikali. Lakini ripoti hizo November 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 4011 ziliwekwa ofisini, na hakuna cho chote kinachofanyika. Ninadhani tutakubaliana sote, kama Wakenya, kwamba Mombasa ni mahali penye hali nzuri ya anga, na haswa pale bandarini. Ukilinganisha Mombasa na bandari zingine, kama vile Dubai, utaona kwamba hali ya anga ya Mombasa ni nzuri zaidi. Kule Dubai, ni vigumu kukaa nje kwa sababu ya joto. Kule Mombasa, unaweza kukaa nje bila shida yoyote. Licha ya hali mbaya ya anga kule Dubai, watu huenda huko kufanya biashara. Watu wa Dubai wamenufaika kwa sababu ya bahari waliyopewa na Mwenyezi Mungu. Dubai hakuna mafuta. Sielewi ni kwa nini tusiige mfano huo na kuitumia bahari tuliyopewa na Mwenyezi Mungu ili tuweze kujipatia senti. Upande wa Likoni peke yake kuna karibu ekari 3,000 za ardhi inayomilikiwa na Halmashauri ya Bandari nchini, KPA. Kama Mbunge wa sehemu hiyo, nina shida kubwa ya kuwazuia watu kuinyakua ardhi hiyo. Tunataka ardhi hiyo iwe wazi, ili mpango huu uweze kufaulu pale utakapotekelezwa. Serikali, au Wizara husika, isipochukua hatua mapema, itakuwa shida kwa Serikali kuipata hiyo ardhi. Pengine, itaibidi Wizara ikanunue ardhi kutoka kwa watu binafsi. Hivi sasa, ardhi hiyo ni bure. Sielewi ni kwa nini tusiitumie nafasi hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine la kuongeza ni kwamba nchi yetu ina haja sana ya kuzalisha nafasi za kazi na pia kuzalisha uchumi. Jambo la kuanzisha bandari huru nchini litatuwezesha kurahisisha mambo haya mawili na kufanya iwezekane hata kupita kiasi kile ambacho Serikali ingefikiria inataka kuandika kazi watu wake. Mimi, kama mkaazi wa Mtongwe, ambapo ni karibu na bandarini, napenda kusisitiza sana umuhimu wa bandari huru kuweko pale. Iwapo tutaanzisha bandari huru, tutakuwa na fursa nzuri sana ya kuwavutia majirani zetu sio tu kuja kununua bidhaa hizi, bali hata kuongezea utalii nchini. Hadi sasa, hapa Kenya tunategemea watalii kutoka nchi za ulaya. Lakini hatujaweza kuwa na motisha ya kuwafanya majirani au Waafrika wenzetu waje kutalii. Watu wengi kutoka nchi za Kiafrika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Burundi na Uganda wanaenda Dubai kufanya biashara huko. Nina hakika kuwa iwapo Bandari ya Mombasa itakuwa huru, bila shaka, watu hawa wataweza kupunguza matumizi au gharama zao za kufika Dubai na kurudi kwao kwa zaidi ya nusu. Kwa hivyo, tutakuwa tunastawisha sio biashara peke yake, bali pia tutaongeza idadi ya watalii pamoja na wale wanaotoka Ulaya. Hali kadhalika, wakaazi wanaokaa sehemu ile, ambao wanafanya biashara ndogo-ndogo, kama vile Bw. Khamisi alivyosema, kwa mfano kuuza chai na kadhalika. Mambo hayo yatawezekana na ule uhalifu ambao unaanza kuzidi huko Mombasa utapungua. Nina hakika kuwa moja katika mambo makubwa yanayotuongezea uhalifu hapa kwetu ni ukosefu wa ajira au kazi ya kumwezesha mtu kuiangalia familia yake. Hakuna mtu yeyote ambaye angependa kuwa mhalifu iwapo kuna nafasi ya kupata riziki. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna jambo la road bypass . Bypass ya Dongokundu ikijengwa, sehemu ya kusini ya Pwani au South Coast na huko Likoni itapanuka, biashara pia zitapata nguvu na ardhi yetu pia itakuwa na thamani. Vile vile, kwa majirani zetu wa Tanzania, tutakuwa tumefungua biashara kati yetu nao, kuliko sasa ambapo wanatumia kivuko cha bahari ambacho kiko mbali sana na hupoteza wakati mrefu sana. Jambo la kufurahisha ni kwamba tuko na wafanyabiashara ambao ni wazaliwa wa Mombasa na Pwani ambao wako tayari kusimamia mpango huu. Pia, wako tayari kupata wafadhili ili kazi hii ifanywe bila ya nchi yetu kutumia pesa zozote ambazo zingetoka katika mfuko wa umma. Hili ni jambo muhimu na sisi, kama watu wa Pwani, tungesisitiza sana kwamba Pwani iwe kielelezo cha maendeleo mapya. Hii sio kusema kuwa jambo hili litatufaidi sisi tu, bali hata Kenya nzima itafaidika pamoja na Wakenya wenyewe. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono kwa dhati Hoja hii. Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}