GET /api/v0.1/hansard/entries/232079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 232079,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/232079/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. L. Maitha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 249,
        "legal_name": "Lucas Baya Mweni Maitha",
        "slug": "lucas-maitha"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia napenda kuunga mkono Hoja hii kwa sababu Bandari ya Mombasa hii leo ni kitega-uchumi muhimu sana katika taifa letu. Hii bandari ni chombo cha taifa hili, na hivi sasa, ni chombo zaidi cha taifa hili. Kama walivyosema wenzangu waliozungumza kabla yangu, Waganda, Warundi na Warwanda 4012 PARLIAMENTARY DEBATES November 29, 2006 wanategemea bandari hii. Hivi sasa, Sudan ya Kusini na hata Ethiopia wanataka kutegemea bandari yetu. Lakini tatizo lililo hapa ni kuwa kwa muda mrefu, Serikali, kupitia Kamati za Bunge na Mawaziri wanaosimamia biashara na uchukuzi wametembea nchi nyingi kuchunguza jambo hili la bandari huru. Na kila anayetoka nje kuona mambo ya bandari huru, anakuja hapa na ripoti ya kuvutia na kusema kwamba, sisi pia ni lazima tuwe na bandari huru. Bw. Naibu Spika wa Muda, hivi leo, shirika letu la ndege la Kenya linafanya biashara kubwa sana kati ya Afrika Magharibi na Dubai kupitia Nairobi kwa sababu ya bandari huru iliyopo Dubai. Kuna msongamano wa watu kwa sababu kila mtu anaelekea Dubai na Singapore kwa sababu ya mambo ya bandari huru. Iwapo Bandari ya Mombasa itakuwa bandari huru, mbali na kuwa itawafaidi watu wale walioko katika eneo lile na taifa zima, pia tuangalie hali ya uchumi ya Wakenya. Wakati mmoja nilibahatika kuwa katika ujumbe wa kuelekea Dubai kuangalia swala hili la bandari huru, na walivyotueleza ni kuwa, mbali na pesa zile zinazopatikana kutokana na bandari, walisema kuwa bandari ile imeweza kuwavutia watu milioni 70 kwa mwaka wanaokwenda huko kwa sababu ya bandari huru. Tukiangalia pesa zinazopatikana kutoka kwa viza ya watu milioni 70 wanaoingia Dubai peke yake kwa sababu ya kufanya biashara katika bandari huru, serikali inafaidika kwa kiasi kipi? Leo, ikiwa tutakuwa na bandari huru Mombasa, uchumi wa Kenya utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika mapato. Hatutakuwa tukitegemea utalii peke yake. Ni kweli kuwa utalii unatuletea pesa nyingi, lakini tumeona kuwa utalii sio biashara ya kutegemea sana, kwa sababu kitu kidogo kinapochapishwa katika magazeti ya Ulaya kinaweza kututatiza. Kwa hivyo, lazima tupanue hali ya biashara mbali na utalii. Laiti leo tungeweza kufanikisha dhana ya bandari huru, taifa hili lingepiga hatua kubwa kimaendeleo. Mimi najua kuwa tatizo linalotufanya tusipate bandari huru ni kuwa Serikali yenyewe imekuwa ikipinga jambo hili. Serikali imejua kuwa vile bandari inavyoendeshwa leo, watu fulani wanafaidika na wanaona kuwa wakibadilisha sheria ili bandari iwe huru, huenda maslahi ya wengine yakatatizwa pale. Hii ndio maana kila wakati tutasema kuwa twataka bandari huru, lakini ikija kwa watu ambao wanatakiwa kuchukua hatua, utaona kuwa hakuna pahali tunapoenda mbele. Sio ajabu kuwa Hoja hii ikipita na baada ya miezi mitatu, Mswada uletwe hapa, tutapata jambo kama lile Mheshimiwa Njoki Ndung'u alikuwa akiuliza; kuwa Hoja yake ilichapishwa, Mswada ukapitishwa na sasa anashtaki tena kuwa Mswada huo hautekelezwi. Nina hakika kuwa tunaweza tukaingia katika maji machafu kwa sababu ya Mswada kama huu. Uzuri wa bandari huru unajulikana. Waheshimiwa Wabunge wanaounga mkono hoja hii wamesema yote ya kusemwa, lakini ombi letu sisi ni kwamba, Hoja hii ikipitishwa, Serikali iwe katika mstari wa mbele ili kuhakikisha kuwa dhana ya bandari huru imetekelezwa kwa kuwa itasaidia taifa letu. Bandari huru itasaidia taifa letu kwa njia mbalimbali. Itasaidia katika upanuzi wa barabara zetu. Pia, itatusaidia kuinua hali ya biashara ndogo ndogo. Nchi nyingi za Africa zitatumia bandari hii kama soko. Wale wote wanaoitumia Bandari ya Dubai watakuja hapa Kenya ikiwa tutaifanya Bandari ya Mombasa kuwa huru. Nchi hii itapata faida nyingi. Hivyo basi, wananchi watafaidika kwa kiasi kikubwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama viongozi tunafaa kuangazia mambo ya bahari katika picha kubwa. Tusione kwamba tukiifanya huru itawafaidi tu watu fulani. Tunaihitaji kwa sasa. Naiomba Serikali kwamba Hoja hii ikipitishwa hapa Bungeni, iwe katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba inatekelezwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}