GET /api/v0.1/hansard/entries/232080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 232080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/232080/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 27,
"legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
"slug": "amason-kingi"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuzungumza juu ya Hoja ambayo imeletwa Bungeni na Bw. Balala. Ningependa pia kuiunga mkono. Naungana na wenzangu kusema kwamba ni muhimu sana kuifanya huru Bandari ya Mombasa. Ni kweli kwamba jambo hili limezungumziwa mara nyingi katika sehemu nyingi. Labda kuna ripoti nyingi ambazo zimeandikwa kuhusu jambo hili. Lakini naamini ya kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Hoja hii November 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 4013 kuja Bungeni. Naamini ya kwamba Bunge linalo uwezo wa kuhakikisha ya kwamba Serikali inatekeleza Hoja ambazo zimepitishwa Bungeni. Kwa hivyo, ninaiunga mkono Hoja hii nikiwa na imani ya kwamba sisi waheshimiwa Wabunge tukiungana pamoja tunao uwezo wa kuhakikisha ya kwamba jambo hili linatekelezwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mji wa Mombasa ni muhimu kwa mambo mengi, kama vile utalii na bandari. Kwa kuifanya bandari hii kuwa huru, tutaongeza dhamani ya Mji wa Mombasa. Tutaufanya uweze kuvutia watu wengi zaidi kuliko vile unafanya sasa. Wengi wanaovutiwa na Mji wa Mombasa labda ni wale ambao wanahusika na mambo ya kitalii au biashara. Lakini tutakapopanua biashara hii ya Mji wa Mombasa kwa kuifanya Bandari kuwa huru, bila shaka tutaongeza kiwango cha biashara. Tukifanya hivyo, bila shaka itabidi tuongeze idadi ya hoteli zetu na mambo mengine mengi ili tuweze kukabiliana na idadi ya watu ambao watautembelea mji huu. Kwa hivyo, hatua ya kuifanya huru Bandari ya Mombasa, itafanya hata vitongoji vya Mombasa pia navyo kuweza kupata mahali pa kufanya biashara ya bidhaa mbalimbali. Leo hii kuna wakulima wanaokuza mboga na wafugaji wengi wa ng'ombe wa maziwa. Hawana soko la mavuno yao kwa sababu idadi ya watu wa Mombasa si kubwa na mikahawa ni michache. Kwa hivyo, mavuno haya, kwa mfano, maembe ambayo yanakuzwa kule Lamu na Kilifi, mara nyingi huwa yanakosa soko kwa sababu idadi ya wanaoyatumia ni ndogo. Lakini tukiifanya huru Bandari ya Mombasa, basi idadi ya wanunuzi itaongezeka. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna ardhi kubwa ambayo imeuzunguka Mji wa Mombasa ambayo haijatumiwa kwa muda mrefu. Tukiipitisha Hoja hii hapa Bungeni, bila shaka itabidi tutumie ardhi hii. Kwa hivyo, wenye ardhi hii nao watapata faida kwa sababu tutainunua au kuikodisha kutoka kwao ili iweze kutumika katika mradi huu. Kutekelezwa kwa mapendekezo ya Hoja hii pia kutaimarisha usafiri. Shirika letu la Ndege la Kenya Airways litapanuka. Itabidi tununue ndege nyingi zaidi ili ziweze kuwasafirisha watu kutoka pembe zote za Africa na dunia kwa jumla, hadi Mombasa kwa sababu ya shughuli nyingi. Itatulazimu tupanue uwanja wa ndege wa Mombasa na viwanja vingine vidogo vilivyoko kule Malindi, Kwale, Kilifi na Lamu. Kuna shirika la reli ambalo limedhoofika kwa sababu ya ukosefu wa biashara nzuri. Bandari ya Mombasa ikifanywa huru, shirika hili litafufuliwa kwa sababu kutakuwa na biashara ya kusafirisha mizigo hadi nchi zingine katika Bara la Africa. Katika Jamhuri yetu ya Kenya, kuna vijana wengi ambao hawana kazi licha ya kuwa na elimu ya juu. Kwa kuifanya huru Bandari ya Mombasa, vijana hawa kupitia hazina ya kuwaimarisha vijana, wataweza kufaidika kwa sababu wataweza kuanzisha biashara zao ndogo ndogo katika sehemu hiyo. Hivyo basi, watapata pesa zitakazowasadia katika maisha yao. Kwa hivyo, hatua hii ya kuifanya Bandari ya Mombasa huru ni muhimu. Ni jambo ambalo limechelewa. Nina imani ya kwamba mara tu Bunge hili litakapopitisha Hoja hii, Serikali italeta Mswada utakaohakikisha kwamba Bandari ya Mombasa inafanywa huru. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}