GET /api/v0.1/hansard/entries/234313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 234313,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/234313/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nitaanza kwa kumpongeza Bw. G.G. Kariuki kwa kuleta Hoja hii ya maana sana ambayo ina faida kubwa kwa nchi hii. Hoja hii ni ya kimaendeleo sana. Vile vile, namshukuru kwa mambo yote aliyosema katika hotuba yake wakati wa kuwasilisha Hoja hii. Iwapo sisi sote, kama viongozi, tutayatilia maanani mambo ambayo amesema, nafikiri tutaweza kupiga hatua kubwa katika kuleta suluhu ya kuboresha maisha ya wananchi wengi katika jamii yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa kumshukuru kwa kumtaja Bw. Karl Marx, ambaye ni mwanzilishi wa ukomunisti wa kisayansi. Hiyo ni sahihi kabisa kwa sababu pale, kuna nadharia maalum kwa Wabunge wote kusoma na kuelewa. Nadharia hizi zinalenga kabisa na kuangalia njia mbali mbali za kutumia ardhi na raslimali vizuri ili kuboresha maendeleo katika taifa lolote lile. Nadhani kwamba watu kama hawa watakuwa wanatajwa mara kwa mara katika Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni muhimu tuunge Hoja hii mkono kwa sababu ina lengo la kuleta Mswada wa kuwatafutia makao watu wasiokuwa na ardhi. Hilo ni lengo muhimu sana. Nikisema hivyo, natambua kwamba hivi sasa, Serikali inaleta mapendekezo ya Sera ya Ardhi. Tumekuwa katika semina hiyo hivi majuzi, na naipongeza Serikali, kwanza, kwa kuanza kufikiria na kuunda mapendekezo ya sera ya ardhi, ambayo yatawasilishwa katika Bunge hili hivi karibuni. Namshukuru Bw. G.G. Kariuki sana kwa kuleta Hoja hii ya kuomba kuletwa kwa Mswada wenyewe. Ombi hili litaiharakisha Serikali kuleta Sera ya Ardhi hapa Bungeni. Vile vile, kutokana na mapendekezo hayo ya sera, kile kinachohitajika ni hatua kabambe za kupambana katika kuleta suluhisho kwa matatizo ya ardhi. Hilo litapatikana baada ya kuleta Mswada kamili. Linalojulikana ni kwamba, matatizo ya kuwa na watu wasiokuwa na haki ya kumiliki ardhi au maskwota ni jambo lililozungumziwa sana katika Bunge hili na katika vikao mbali mbali, siku nenda, siku rudi. Hatuwezi kuendelea kuzungumza milele. Ndio maana Hoja hii ya Bw. G.G. Kariuki na hotuba yake inavyosema. Lazima tuanze sasa kutafuta suluhisho. Naunga mkono maoni ya Bw. G.G. Kariuki kwamba, sisi kama Wabunge na vile vile Serikali iliyoko, ina uwezo, kama inataka, ya kuleta suluhu. Ni kweli kwamba Serikali yoyote ambayo italeta suluhu katika maswala ya ardhi, haswa katika kuhakikisha kwamba kila mwananchi atafaidika kutokana na ardhi na raslimali zilizoko katika nchi hii, hiyo Serikali ndio itakayokuwa ya kwanza kuanza kushughulikia maslahi ya nchi na kuleta maendeleo kwa ujumla. Nasema hivi 3664 PARLIAMENTARY DEBATES November 15, 2006 kwa sababu hatuwezi kuwa nchi huru kama ardhi yetu inatawaliwa na wageni. Kwa mfano, ukienda Pwani, utaona kuwa hoteli nyingi zinamilikiwa na watu kutoka nje. Hawa ndio wanaofaidika sana, haswa kutokana na faida hiyo ya ardhi iliyoko kando kando ya bahari. Vile vile, ukienda katika sehemu zingine humu nchini, iwe ni Laikipia, Taita-Taveta ama wapi, utakuta kuwa watu wengi kutoka nje wamepewa uhuru kutumia raslimali zetu zilizoko hapa za ardhi kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Hatuwezi kusema kwamba tuko huru kwa njia hiyo. Vile vile, hatuwezi kuwa na maendeleo na haki iwapo kuna idadi kubwa ya wananchi wetu ambao hawana hata inchi moja ya ardhi yao. Hatuwezi kusema kwamba tuko huru kwa njia hiyo. Hatuwezi kuwa na maendeleo tukiwa na idadi kubwa ya wananchi wasiokuwa na mashamba. Hatuwezi kuwa na usalama nchini. Vita vya kikabila vinavyotokea katika sehemu mbalimbali hapa nchini vinatokana na umasikini na ukosefu wa mashamba. Watu wengi hawana mashamba ya kuwafugia wanyama wao. Ikiwa kila mmoja wetu atamiliki shamba, basi hili litakuwa ni suluhisho la shida ya usalama nchini. Tunafaa kuwa na sheria maalum ambayo inatokana na mapendekezo ya Hoja hii. Badala ya kusuluhisha matatizo ya maskwota, tunawaongeza. Mfano mmoja ni Wilaya ya Taita-Taveta. Kuna madini mengi katika wilaya hii. Pia kuna rasilimali kama vile wanyama pori na maji. Badala ya hifadhi ya wanyama wa pori kupunguza ardhi inayomiliki, hivi sasa inataka kuongeza ardhi hiyo. Hivyo basi, kuna matatizo baina ya wenyeji wa sehemu hiyo na Serikali. Vile vile kuna watu binafsi wanaokubaliwa na Serikali kumiliki mamia ya ekari ya ardhi yenye rasilimali ya madini. Hatua hii imewafanya watu wengi waendelee kuwa maskwota. Kuna ufisadi wilayani unaoongozwa na wakuu wa ofisi za arthi na makao. Wao ndio wanaogawa hayo mashamba. Vita vingi vinavyotokea katika wilaya mbalimbali hapa nchini vimechochewa na makao makuu ya wilaya hizo. Kwa hivyo, Waziri wa Ardhi akitaka kusuluhisha matatizo ya mashamba katika Wilaya ya Taita-Taveta, anafaa kumtembelea Mkuu wa Wilaya na kumkanya dhidi ya kuendelea kuwaruhusu watu binafsi kuendelea kunyakuwa ardhi ya watu wetu. Vile vile, anafaa kumkanya dhidi ya kuruhusu Mbuga ya Wanyama ya Tsavo kuendelea kunyakua ardhi zaidi kutoka kwa watu binafsi. Jambo hili limesababisha kuongezeka kwa maskwota. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa jumla, Hoja hii inahitajika mara moja. Nataraji Bunge hili litaunga mkono Hoja hii ili tuweze kusuluhisha tatizo la maskwota nchini. Tukifanya hivyo, tutaondoa umasikini katika nchi yetu. Vile vile hatua hiyo itapunguza kuenea kwa mitaa ya mabanda inayoongezeka kila siku katika miji yetu. Jiji la Nairobi ni chafu sana kiasi cha kwamba tunashangaa kama kweli tuna Serikali au la. Wageni kutoka nchi zingine wakitembelea jiji hili wanashangaa kama kweli tuna Serikali au la. Pia kuna nyumba zinazoendelea kujengwa kiholela. Ardhi imenyakuliwa na mabepari wachache na hata makanisa. Makanisa yamepoteza maadili ya kidini. Hatuwezi kupanga miji yetu kama hatujalitatua tatizo la ardhi na kuwapa maskwota mashamba. Vile vile tunafaa kuunda sera maalum inayosimamia mambo ya umiliki wa ardhi hapa nchini. Naomba Bunge hili liunge mkono Hoja hii. Baada ya kuipitisha Hoja hii, Serikali inafaa ilete mara moja Mswada wa mapendekezo ya sera za ardhi. Ikifanya hivyo, suluhisho la tatizo la maskwota litapatikana. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}