GET /api/v0.1/hansard/entries/234356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 234356,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/234356/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi waakilishi wa Serikali upande huu tumesikia na tutafikisha ujumbe huo kwa wakubwa wetu. Ni matumaini yangu kwamba mudawangu wa kujibu Hoja hii bado upo. Nilikuwa nikisema ya kwamba Serikali hii haiwezi kupinga Hoja ambayo inaambatana na matakwa na malengo yake. Isitoshe, Bw. G.G. Kariuki, aliyewasilisha Hoja hii, anataka Bunge hili limpe ruhusa ya kuwasilisha Mswada hapa ambao utahakikisha ya kwamba maskwota miongoni mwetu wamepata makao. Wakati tulikuwa tunaijadili Hoja ya Katiba mwaka uliopita, moja ya maswala ambayo yalikuwa katika Katiba kielelezo, ni swala la maskwota. Serikali iliunga mkono Katiba hiyo kwa sababu ilikuwa na imani na bado ina imani ya kwamba kuna haja kubwa ya kuwapa maskwota makao. Bw. Naibu Spika wa Muda, juzi Mheshimiwa Rais alizuru Mkoa wa Pwani, na kuwapa maskwota hati za kumiliki mashamba. Tunaelewa ya kwamba maskwota wako kila pahali nchini na tunahitajika kuwashughulikia wote. Tunataka maskwota nchini wapewe mashamba na hati za kuyamiliki. Hati hizi zitawasaidia kumiliki mashamba hayo milele. Bw. G.G. Kariuki amefanya kazi nzuri kwa kuleta Hoja hii. Nikiongea kama Mbunge wa kawaida, ninakumbuka ya kwamba katika mwaka wa 2003, nilileta Hoja hapa juu ya swala la maskwota. Nilitaka Serikali iwashughulikie na kuwapa makao maskwota katika nchi hii. Hoja hiyo ilipitishwa. Lakini, kwa bahati mbaya, hadi sasa, mapendekezo ya Hoja hiyo hayajawahi kutekelezwa. Wakati huu, Bw. G.G. Kariuki amechukua hatua ya kuja hapa na kuomba ruhusa ili auwasilishe Mswada ambao utakuwa sheria. Ninampongeza kwa kuchukua hatua hii muhimu sana. Iwapo tutapitisha Hoja hii na baadaye alete Mswada na pia tuupitishe, basi tutakuwa na sheria ambayo itahakikisha ya kwamba hakuna skwota nchini ambaye ataishi bila bila makao. Ni lazima tumpongeze Bw. G.G. Kariuki kwa kuchukua hatua hiyo mwafaka. Nafikiri ya kwamba waheshimiwa Wabunge wanastahili kujifunza somo kubwa kutokana na hatua hii. Hii ni kwa sababu wakati mwingi Hoja huletwa hapa, tunazijadili na kuzipitisha na kisha hazitekelezwi. Ni 3674 PARLIAMENTARY DEBATES November 15, 2006 muhimu kuhakikisha ya kwamba Hoja inapata \"meno\". Hoja haiwezi kupata \"meno\" hadi itakaporudi hapa kama Mswada. Mswada huzaa sheria. Haya mengine ni kama ya kupitisha wakati tu. Bw. Naibu Spika wa Muda, swala la maskwota nchini Kenya lina historia ndefu. Nimesikia wengine wakiuliza ni kwa nini inakuwa hivyo? Ni kwa nini tumekuwa na maskwota hata baada ya sisi kuupata Uhuru? Nadhani watu wana majibu tofauti kwa swala hili. Ninaamini ya kwamba swala la maskwota lilipata mizizi baada ya Uhuru wakati sisi tulipoamua kuufuata mfumo wa ubepari; tofauti na ule wa ujamaa. Najua katika Bunge hili tuna wafuasi wengi wa mfumo huo wa ubepari na ambao wanaweza kusema hicho si chanzo cha tatizo hili. Ni lazima tuelewe ya kwamba ubepari ni mfumo ambao unashikilia ya kwamba kuna watu wenye haki na wengine ambao hawana haki. Ni lazima watu wetu wawe na haki ya kumiliki mali na mashamba, bali na zile haki za kibinafsi. Ukifanya uamuzi huo; ya kwamba unataka msingi wa maendeleo wa nchi uwe ni falsafa hiyo ya ubepari, basi, tupende tusipende, kutakuwa na tofauti hizi ambazo tunajadili hapa. Tuliambiwa na Bw. G.G. Kariuki ya kwamba Uhuru ulicheleweshwa kwa kwa muda wa miaka miwili hivi wakijadili swala la mashamba. Hata hivyo, hakutueleza hasa walikuwa wanasema nini wakati wa majadiliano hayo. Nahisi ya kwamba ni Wazungu ambao walikuwa wakitetea haki yao ya kuendelea kumiliki mashamba baada ya Uhuru. Walifaulu kwa sababu kuna Wafrika wengine ambao walikubaliana nao, mradi tu wangeweza kuungana mikono na kujenga umoja wao wa kumiliki mashamba na huko mamilioni ya watu wetu wabaki bila mashamba. Kwa watu hao, huo ulikuwa ni mpangilio sawa sawa. Hii ndiyo sababu tulipopata Uhuru, Serikali ya hayati Mzee Jomo Kenyatta na hata ile Rais Mtaafu Moi, ziliendeleza mfumo wa kikoloni au upebari. Huo ndio mfumo tunaoutafutia jawabu. Kama hatukujibu swala la falsafa ya nchi; aidha kama tutakuwa watu ambao wanafuata ujamaa, hata kama ni ule wa Kiafrika, tuendelee kushikilia huu mfumo wa ubepari. Hatutaka kuyajadili mambo haya kwa makusudi. Hatukutaka kuwa na jawabu ya swali hili lenyewe. Jawabu letu lingekuwa utekelezaji wa falsafa ya ujamaa wa Kiafrika. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukweli wa mambo ni kwamba nchi hii ni yetu sote. Hatuwezi kuwa na nchi ambapo watu wachache wanamiliki mashamba na wengine wetu hawataruhusiwa kumiliki hata kipande cha ardhi. Sote tu sawa na tuna haki ya kumiliki ardhi hii. Nasema hivi kwa sababu kukazuka vita leo watakaoajiriwa kazi ya kulinda nchi hii, wengi wao watakuwa ni maskini. Unakumbuka kwamba wazungu walikuwa na taratibu ambayo tunafaa wakati mwingine kuitazama na kuifuata. Wakati wazungu waliwapeleka watu wao kupigana katika Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, wakati waliporudi, waliwatunza kwa kuwapa maekari ya mashamba kwa sababu ya kutetea himaya yao. Wazungu hawakuwa wakinyakua mashamba kwa niaba ya watu wengine. Ninachosema ni kwamba waliwapa watu wao zawadi za mashamba. Ninaamini ya kwamba, nchi hii haiwezi kulindwa na matajiri peke yake. Kwa hivyo, kuna haja ya kuwashughulikia masikini ambao tutawategemea kulinda nchi wakati wa vita. Ni lazima tuwape nafasi ya kumiliki mashamba katika nchi hii. Wasipomiliki mashamba katika nchi hii, watamiliki wapi kwingine? Hata hatuna uhakika ya kwamba mbinguni kuna mashamba. Naona kama ni hali tupu. Sijui kama kuna mashamba kule. Kwa hivyo, kama mtu hajamiliki shamba akiwa hapa duniani hawezi kumiliki pahali pengine. Ni lazima tukubali ya kwamba swala hili si kama lile linalosimuliwa katika riwaya ya Shamba la Wanyama, pahali ambapo wanyama wote ni sawa, lakini wengine ni sawa kuliko wengine. Hii ni nchi ambayo inastahili kutuunganisha sisi sote, maskini kwa matajiri. Ni lazima watu wa tabaka zote waunganishwe ili kila moja wetu ajivunie kuwa Mkenya. Hatutaki wengi wetu kuvumilia kuwa Wakenya. Wengi wetu wanavumilia kwa sababu wamelemewa. Tunataka kujivunia kuwa Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, baada ya kuangalia maslahi ya maskwota wa Mkoa wa Pwani, tungependa Serikali ishughulikie maskwota katika sehemu zingine hapa nchini. Pahali ambapo November 15, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 3675 panastahili kupigwa darubini ni kule ambako watu walitimuliwa kutoka kwa mashamba yao wakati wa vita vya kikabila. Watu hawa, mpaka wa leo, bado ni wakimbizi katika nchi yao. Wamejaa kila pahali. Ikiwa tuna mashamba chungu nzima ambayo yalinyakuliwa na wageni--- Kwa mfano, limetajwa shamba lile la Lord Delamere, katika Wilaya ya Nakuru, pahali ambapo mara nyingi nimejihisi kama mgeni ambaye anapitia nchi ya mtu mwingine. Ukienda huko Laikipia utakuta kwamba hali ni hiyo hiyo. Maekari ya mashamba yanamilikiwa na wageni. Ukienda kule Sotik, hali ni hiyo hiyo. Kwa hivyo, hatuwezi kulia eti hatuna mashamba ya kuwapatia watu. Watu waliofukuzwa kutoka makwao ni muhimu watafutiwe makao wakati huu. Mimi ninaamini kwamba ikiwa sisi tulio Serikalini kweli tunataka kurudi Serikalini, ni muhimu tulishughulikie swala hili. Ninayo imani kuwa tutalishugulikia kabla ya mwezi wa Desemba ili tuweze kupigiwa kura na kurudi uongozini. Hatuna jingine la kufanya sasa ila kuwashughulikia maskwota ili tuweze kushikilia hatamu za uongozi tena. Hakuna cha bure kabisa. Watu hawawezi kukupigia wewe kura ilhali hutumizi wajibu wako ama hutimizi agano. Wananchi wanapotuchagua, agano huwa hivi: \"Tunawachagua ili nanyi mtutafutie makao.\" Sisi tutalitimiza agano hilo."
}