GET /api/v0.1/hansard/entries/234366/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 234366,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/234366/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nasema kwamba wizi wa mashamba uko pahali pengi na siyo tu katika maeneo ya misitu. Mimi ninatoka Subukia, ambako kwa miaka mingi, watu ambao walikuwa wanachama katika makampuni yaliyonunua mashamba kutoka kwa wazungu ili yaweze kuwagawia Waafrika, wamekosa mashamba. Watu walinyang'anywa mashamba yao wakati wa utawala wa giza katika nchi hii. Ingawa watu walinunua hisa katika makampuni kama vile Ngwataniro, Ndeffo au Kihoto, watu hao wanashikilia stakabadhi za mashamba yao lakini hawana mashamba yenyewe kwa sababu walinyang'anywa. 3676 PARLIAMENTARY DEBATES November 15, 2006 Ingawa tunaongea kwa niaba ya Serikali, tungetaka Wizara ya Ardhi ielewe kwamba ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wale walionyang'anywa mashamba yao bado wanangojea kurudishiwa mashamba yao. Si watu wachache; ila tu hawana nguvu. Ufisadi unaowaathiri hauwezi kuandikwa na vyombo vya habari kwa sababu ni watu wadogo. Hata hivyo, Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba imewasaidia kupata mashamba yao ili nao wajihisi kama Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, ingawa tunaongea juu ya maskwota, inawapasa nao kuelewa kwamba wana wajibu wa kusaidia katika kusuluhisha swala hili. Wanaweza kufanya hivyo kwa kuchagua watu ambao si wezi wa mashamba wakati wa uchaguzi. Maskwota wasiwe watu wa kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe kama nguruwe. Utagundua, kwa mfano, wakati wa mjadala kuhusu Katiba mpya, wananchi wengi waliikata Katiba hiyo ingawa ingewasaidia kupata mashamba. Wakati wa uchaguzi ujao, utaona wananchi hao wanaoteseka wakiwachagua wanyakuzi wa mashamba kama viongozi wao. Sasa, wakiwachagua wanyakuzi wa mashamba kuwa viongozi wao, ni vipi watajisaidia? Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}