GET /api/v0.1/hansard/entries/234523/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 234523,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/234523/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Karume",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 234,
"legal_name": "Njenga Karume",
"slug": "njenga-karume"
},
"content": " Bw. Naibu Mwenyekiti wa Muda, ningependa kuunga mkono pendekezo lake mhe. Bifwoli kwa sababu mimi nilimfahamu vema hayati Masinde Muliro. Yakini, kama kuna mtu alipigania haki za nchi hii basi ni hayati Masinde Muliro. Wakati ambapo wabeberu walikuwa wamekatalia humu nchini, ile kazi ambayo hayati Masinde Muliro alifanya ilikuwa muhimu sana. Yeye, hata akiwa huko Kitale, hakuwa mkabila. Labda itakuwa vema ikiwa tutatenga mahali pakuweka picha na majina ya mashujaa ambao walipigania Uhuru wa nchi hii wakiongozwa na hayati Mzee Jomo Kenyatta. Ninayo imani kuwa jina lake hayati Masinde Muliro litawekwa katika kumbukumbu hiyo. Kwa hayo machache, naunga mkono pendekezo kwamba hiki chuo kikuu kiitwe jina lake. Aidha, siku za usoni, tuweze kubuni namna ya kumkumbuka hayati Masinde Muliro hapa Nairobi."
}