GET /api/v0.1/hansard/entries/235981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 235981,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/235981/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Dzoro",
    "speaker_title": "The Minister for Tourism and Wildlife",
    "speaker": {
        "id": 247,
        "legal_name": "Morris Mwachondo Dzoro",
        "slug": "morris-dzoro"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nasimama hapa kuunga mkono Mswada ulioko mbele yetu. Nashukuru kwa sababu hivi tunavyoongea, Wakenya wengi katika sehemu za mashinani huko mashambani wamekuwa wakiteseka sana, hasa makundi ya akina mama. Tunafahamu kuwa kuna makundi ya akina mama katika nchi hii ambayo yameundwa kwa ajili ya kupunguza umaskini, na wanakutana kila wiki kutoa hela kidogo za kuwasaidia. Inaonekana kwamba hili ni jambo ambalo halitaendelea sana kwa sababu, mwisho, tuemeona kwamba hela hizo huangukia kwenye mikono mibaya na kutumiwa vibaya, na baadaye, akina mama wale hushindwa kuendelea na mipango yao. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu kwa sababu utasaidia nchi yetu. Kwa wakati huu, matajiri wana nafasi kubwa kuliko maskini, haswa katika kupata mikopo. Wale ambao wanaishi katika miji ndio wamekuwa na bahati kwa sababu benki zote kubwa kubwa ambazo zinaweza kuwasaidia zimo humo. Vile vile, wale ambao wana stakabadhi za mashamba ndio wanapewa mikopo ya kuendeleza biashara zao. Bw. Naibu Spika wa Muda, huu ni wakati mzuri Mswada huu upitishwe mara moja ili wale walioko mashambani; kwa mfano, akina mama na vijana, wapate nafasi ya kuendeleza maisha yao kama wale wengine. Ikiwa utajiri utasambazwa kule mijini na mashinani, nchi yetu itaendelea. Leo hii, ukienda kule vijijini, ukitaka upate sarafu ndogo ndogo za Kshs1,000, utazunguka katika maduka mengi, lakini huwezi kupata kwa sababu hela haziko vijijini, bali zipo katika miji mikubwa mikubwa. Naona kuwa Mswada huu utaweza kutusaidia ili pesa ziweze kusambaa kila mahali nchini kwetu. Kuna watu ambao ni magaidi, ambao wamechukua nafasi hiyo na kujifanya kuwa wao ndio watawakopesha watu pesa ili wapate faida. Mwishowe, watu hao huchukua vitu vya watu na kuvinadi kwa sababu wameshindwa kulipa ile riba iliyotakikana. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu umekuja wakati mzuri. Nami naunga mkono na kuomba tuuptishe mara moja ili watu wetu waweze kunufaika. Kwa sababu naona kuna waheshimiwa Wabunge wengi ambao wanataka kuchangia Mswada huu, nami nataka upitishwe haraka, kwa hayo machache, naunga mkono. Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}