GET /api/v0.1/hansard/entries/236304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 236304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/236304/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye alitujalia elimu kupitia ufunuo na uhusiano kupitia Mitume, kati yao akiwa Mtume wa mwisho Mohammed, ambaye katika ufunuo wake wa kwanza kwa mitume, aliwaambia, \"soma.\" Neno soma ni tendo ambalo halifungamani na wakati au umri. Hivyo basi, utu au kufaulu kwa mtu duniani kunategemea kusoma kwake au uwezo wa mali aliyo nayo. Kamwe, sitasahau kumpongeza Waziri na Serikali kwa kukumbuka na kusajili au kuleta Mswada wa kusajili chuo kikuu cha WUST. Ingawa amechelewa, bado tunampongeza Waziri. Kuna vifungu kama vile 5(10) na vingine ambavyo tuna matatizo navyo. Hivyo nitavijadili wakati Mswada huu utafika mbele ya Kamati. Kenya inataka vyuo vikuu, si sita, bali zaidi ya 60. Kwa nini nimesema hivyo? Utapoangalia sera ya elimu iliyo katika Kenya leo; ya kutoa elimu bila ya malipo, imewasaidia watoto wa darasa nane, idadi 660,000. Baada ya miaka michache ambayo inakuja, tutalenga watoto zaidi ya milioni moja. Je, watoto hao wataelekea wapi baada ya kumaliza elimu yao ya shule ya msingi na ya upili? Kwa sababu ya uchache wa vyuo vikuu katika nchi hii, elimu ya vyuo hivyo imekuwa ya watoto wanaotoka katika jamii tajiri. Maskini hawapati fursa ya kujisajili kwa chuo kikuu kwa sababu hali yao ya mapato haswa ya kifedha ni ngumu kwao. Gharama ya vyuo vikuu iko juu sana na jamii maskini haziwezi kuimudu. Kuna changamoto nyingi ambazo zinafaa kufanyiwa utafiti. Hadi leo, hatuna muongoza kamili wa utafiti. Tunatoka katika sehemu kame, sehemu ambayo haina uhakikisho wa chakula. Je, ni haki kutumia viini tete? Adhari ya viini tete kwa mwili wa binadamu na ardhi ni nini? Kuna maswala mengi yakiwemo ya kimazingara ambayo tunafaa tuyaangalie. Kuna miti ambayo inaitwa Prosopis Juliflora ambayo ililetwa kutoka nchi za ng'ambo. November 7, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 3449 Ukosefu wa utafiti baina ya maprofesa wetu ndio uliofanya watu kuleta miti hiyo ambayo ni tisho kwa maisha ya watu wetu wanaoishi katika sehemu kavu. Hayo ndiyo baadhi ya maswala ambayo yanafanya tutake idara za utafiti kuanzishwa. Utafiti hufanywa tunapokuwa na vyuo vikuu na mapato ya kutosha. Kisha, ari yetu inaamshwa, tunatiwa tamaa, dakika ya mwisho tunaambiwa hakuna mafuta katika nchi yetu. Ni lini tutakuwa na watafiti wetu ambao wataenda kufanya uchunguzi kama huo? Haya tutaweza kuimudu iwapo tutakuwa na vyuo vikuu vya kutosha. Tunapozungumza sasa, zaidi ya asilimia 90 ya watoto wetu wanatafuta elimu ya vyuo vikuu kutoka nchi za nje. Ujiulize, mtoto mmoja anatoa senti ngapi kutafuta elimu hii? Ikiwa asilimia 90 wanasomea nje, wanapeleka pesa ngapi nje? Ni kwa nini tusitumie changamoto kama hicho kuboresha hali ya uchumi ya nchi hii? Bw. Naibu Spika wa Muda, baraza linaloshughulikia usajili wa vyuo via umma na via kibinafsi lisifanye ubaguzi linaposajili vyuo vikuu. Ninasema hivyo kwa sababu zaidi ya miaka saba leo, chuo cha kiislamu cha Thika kimeomba usajili lakini mpaka leo hakijasajiliwa."
}