GET /api/v0.1/hansard/entries/236307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 236307,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/236307/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninasema kwamba baraza la vyuo vikuu lisifanye ubaguzi wakati wanaposajili vyuo vikuu. Ninasema hivi kwa sababu sasa ni zaidi ya miaka saba tangu chuo kikuu cha kiislamu cha Thika kiombe usajili. Ukiangalia makanisa karibu yote leo yana na vyuo vikuu vyao. Kwa nini kusiwe na chuo kimoja kwa jamii ya waislamu ili nao waweze kuendeleza shughuli ya dini yao? Hii imelazimu watoto wengi wa kiislamu waende Sudan, London ama Uganda kutafuta elimu. Mbona Serikali inatuweka kwa gharama hii na sisi tuko na chuo hapa ambacho kinaweza kufaidi watoto wetu? Bw. Naibu Spika wa Muda, nitarudia kuhimiza Waziri afikirie kuteremsha kiwango cha watoto kuingia vyuo vikuu. Ninasema hivi kwa sababu ukiangalia maprofesa wengi, akiwemo mashuhuri kabisa, Prof. Ali Mazrui, hakufanya vizuri katika kidato cha nnne. Lakini alipopata fursa, Prof. Mazrui anatambulika leo katika nyanja ya kielimu. Watoto wanaotoka katika sehemu kame, kwa sababu ya ukosefu ya karakana hawawezi kushindana na watoto wengine. Ninauliza Waziri aangalie sehemu hiyo na aboreshe hali hiyo. Jambo la mwisho, iwapo Serikali inataka kufaulu kwa watoto wetu, ni lazima iangalie masilahi ya wahadhiri wa vyuo vikuu. Tumesikitishwa na vile Wizara imeshughulikia swala la wahadhiri. Mishara yao lazima iboreshwe. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}