HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 236955,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/236955/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nitaanza kuzungumza nikimpongeza Mbunge wa Bahari kwa kutambua umuhimu wa kulishughulikia swala la maskwota nchini, na haswa kuzingatia shida tuliyo nayo mkoani Pwani ya watu wetu walionyanganywa ardhi yao na kugandamizwa kuanzia nyakati za ukoloni wa Mwarabu na ukoloni wa Mzungu, hadi wakati huu ambapo ukoloni mambo leo unaendelea. Hii ni Hoja muhimu sana. Ninashukuru kwamba Hoja hii imeletwa Bungeni wakati ambao Serikali pia imependekeza Sera mwafaka kuhusu ardhi ambayo inaendelea kutayarishwa na Wizara ya Ardhi. Sera hiyo inaambatana na Hoja hii. Ningependa kusema kwamba wale tunaoiunga mkono Hoja hii tutaendelea kuiunga mkono Sera ya Serikali kuhusu ardhi, tukisisitiza kwamba wakati umefika kwa Serikali iliyopo, au Serikali yoyote itakayofuata, kuamua iwapo itazingatia maslahi ya wengi, ambao wananyanyaswa, ama yale ya wachache. Kwa sababu Serikali haijawahi tayarisha Sera kakamavu na kuzitekeleza kwa ukakamavu ili kulitatua tatizo hili, ni wazi kwamba Serikali bado inawatumikia wale walio wachache. Ninasema hivyo kwa sababu, kila wakati swala la maskwota linapoibuka, sheria ya kulinda mali ya watu binafsi hutumiwa na Serikali sana, dhidi ya watu walionyanganywa ardhi yao. Sijaona sheria hiyo ikitumiwa kuwaunga mkono wale walionyanyaswa. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeshuhudia mara nyingi maskwota, ambao wameishi katika ardhi kwa miaka mingi bila mtu yeyote kujitokeza kudai umiliki wa ardhi hiyo, wakiondolewa kutoka makao yao. Tumewaona maafisa wa Serikali wakisema kwamba maskwota hao waondoke katika ardhi hiyo, kulingana na sheria. Ningependa kuona wakati tutakapokuwa na kiongozi mwenye ujasiri sawa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika nchi hii, ambaye atasimama imara na wananchi, dhidi ya madola, na kutekeleza sera mwafaka kwa lengo la kuleta marekebisho ya kimapinduzi kuhusu swala la ardhi katika nchi hii. Huo ndio wakati tutakaposema kwamba, kweli, tuko na Serikali ambayo imeamua kuleta mabadiliki humu nchini. Tutakapokuwa na viongozi wenye ujasiri sawa na Rais Morales wa Bolivia na Rais Chavez wa Venezuela, tutaamini kwamba kweli tumepata mashujaa wa kuwatumikia Wakenya. Huo ndio wakati ambapo swala la ardhi litazingatiwa kikamilifu. Tukiendelea kutumia zile sheria zilizokuwa zikitumika kuanzia wakati wa ukoloni wa Mwarabu, hatutalitatua tatizo hili. Mwarabu alipowasili Pwani, aliwauliza wenyeji iwapo walikuwa na hati za umiliki wa ardhi. Ilisemekana kwamba wenyeji wa ukanda wa pwani hawakuwa na ardhi eti kwa sababu hawakuwa na hati za umiliki wa ardhi. Bw. Naibu Spika wa Muda, hivyo vipande vya karatasi ndivyo vinavyotumiwa katika nchi hii kuwanyanganya maskini ardhi yao. Hata tunapozungumzia hivyo vipande vya makaratasi, tusiwe wenye kusifu sana hati za umiliki wa ardhi ama kuviheshimu sana hivyo vipande vya makaratasi, kwa sababu hati hizo za umiliki wa ardhi ndizo zinazotumiwa kuwanyanganya watu wengi ardhi yao. Ninapendezwa sana na Hoja hii, kwa sababu inalitaka Bunge kuiomba Serikali itumie mbinu zote zinazohitajika ili kuwapatia wananchi ardhi ambayo haijakaliwa na watu wanaodai kuimiliki. Miongoni mwa mbinu hizo ni pamoja na kutumia nguvu za dola. Siyo kutumia sheria peke yake na kupoteza pesa za umma tukinunua ardhi ya watu ambao hata hawamo humu nchini, 3298 PARLIAMENTARY DEBATES November 1, 2006 kama tulivyoona bepari mmoja, Waziri wa Serikali, aliyeiuzia Serikali ekari 40 za ardhi, ambayo hapo awali ilikuwa ardhi ya umma, na kujipatika Kshs280 milioni. Ni lazima njia zote zitumike kuhakikisha ya kwamba haki inatendeka kwa watu ambao mashamba yao yalinyakuliwa. Nazungumza jambo hili nikiwa na uchungu mwingi kwa sababu mimi ni mwenyeji wa Wilaya ya Taita Taveta. Ni aibu kuwa asilimia 60 ya ardhi katika wilaya hii, imo mikononi mwa mbuga za wanyama za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi. Asilimia 20 ya ardhi nayo imo mikononi mwa mabwenyenye. Mabwenyenye hawa wana maelfu ya ekari za ardhi. Sehemu inayosalia, ambayo ni asilimia 12, ni mawe, misitu, nyumba za Serikali na shule. Watu wetu wamerundikana katika asilimia nane ya ardhi. Ni jambo la kuhuzunisha kuona ya kwamba hata ardhi hii ya asilimia nane, mabwenyenye wanainyemelea. Kuna pia matajiri wanaofanya shughuli za kuchimba madini na wengi wana mashamba makubwa ya makonge. Watu wetu hawana ardhi ya kutosha. Mashamba haya yanaponyakuliwa, wakuu wa wilaya wanaketi kitako na kutazama tu! Watu wa eneo langu la Wundanyi na Wilaya ya Taita Taveta kwa ujumla wanataka kuona haki imetekelezwa. Wao husema: \"Tunataka tuongezewe asilimia nane ya ardhi, sio kupunguziwa\". Mara kwa mara, Serikali inachukuwa msimamo wa watu wanaonyakua ardhi kwa niaba ya mahoteli, wachimbaji madini na wanaofuga wanyama. Bw. Naibu Spika wa Muda, la muhimu kusisitiza ni kwamba mapendekezo mengi katika sera hii yamo na Wizara ya Ardhi na Makao. Hakuna mambo mageni katika sera hii. Ada ya mja husema: \"Mungwana ni kitendo.\" Kwa hivyo, tutathmini Serikali hii kwa matendo yake halisi ya kuleta suluhuhisho juu ya mambo haya ya ardhi. Kuna matajiri wanaodai kuwa na ardhi kubwa katika Mkoa wa Pwani lakini hawaipendelezi. Wengi wao hudai ni mali yao. Hata hivyo, hawajawahi kuonekana hata siku moja. Serikali inafaa ifanye haraka kusuluhisha jambo hili. Tukisema tutafuata njia ya kisheria, tutakuwa tunafukuza upepo kama swala la ufisadi, hasa lile la Anglo Leasing au Goldenberg. Hizo sheria zitatea wezi wengi. Inafaa tuwe na kitendo halisi kama kile kilitumiwa kuchukua jumba la Kenyatta International Conference Centre (KICC) kutoka kwa chama cha KANU ambacho kilikuwa kimenyakuliwa kutoka kwa wananchi. Vitendo vya namna hiyo, ndivyo vinaweza kuleta suluhuhisho kwa shida kama hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu inapendekeza haki itekelezwe kwa maskwota wote, hasa wa Mkoa wa Pwani na wanaoishi vibandani."
}