GET /api/v0.1/hansard/entries/237011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 237011,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237011/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Dzoro",
"speaker_title": "The Minister for Wildlife and Tourism",
"speaker": {
"id": 247,
"legal_name": "Morris Mwachondo Dzoro",
"slug": "morris-dzoro"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Bw Khamisi, ambaye ameileta Hoja hii Bungeni. Kusema kweli, haya ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Dini zote zinasema kwamba, katika mambo ambayo ni ya urithi wa mwanadamu tangu alipoumbwa, ardhi ni kitu cha maana November 1, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 3313 sana. Mwanadamu mwenyewe ameumbwa kwa mavumbi. Kwa hivyo, ni jambo la kuhuzunisha kwamba licha ya kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia mwanadamu aitunze ardhi, katika sheria za kibanadamu, wanadamu wengine wamelichukulia jambo hilo kwa hali isiyofaa, haswa tukizingatia historia ya Kenya, na haswa kuhusu Mkoa wa Pwani. Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi, watu wa pwani, tumepata shida sana kuhusu ardhi. Kwa hivyo, Hoja hii imeletwa Bungeni wakati unaofaa. Ningependa kuhimiza kwamba mambo haya yafanywe haraka iwezekanavyo ili watu wapewe vyeti vyao vya kumiliki ardhi, na wale watu ambao wako na mashamba lakini hawayalimi, wapewe nafasi ya kuyalima mara moja ili chakula kipatikane haraka iwezekanavyo. Vile, kuna sehemu ambako watu hawawezi kufanya makao kwa sababu hakuna maji. Kukiwa na mpangilio maalum wa kupeleka maji katika sehemu hizo, watu wanaweza kuanzisha shughuli za uzalishaji vyakula bila ya wasiwasi.Ninaiunga mkono Hoja hii kwa moyo wangu wote."
}