HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 237710,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237710/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Capt. Nakitare",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kuniruhusu kuchangia Hoja hii ambayo inahusu usawa wa jinsia na maendeleo. Wakati Serikali ilianza kuzingatia usawa wa jinsia, Wizara hii ilikuwa inawahudumia vijana na walemavu. Wakati huo, Wizara hii haikuzingatia mambo ya jinsia. Ilijihusisha sana na michezo na utamaduni. Hivi sasa, inajishughulisha sana na jinsia, michezo, utamaduni na huduma kwa jamii. Hoja hii inapendekeza Wizara hii izingatie usawa wa jinsia na maendeleo. Hii ni kwa sababu historia ndio msingi maalum wa siku za usoni. Mwaka wa 1975, marehemu Rais mwanzilishi wa Taifa hili, alianzisha mradi wa walemavu. Miradi mingi ilianzishwa ili kuwasaidia walemavu. Hivi sasa tunafaa kutafuta njia zaidi za kuwasaidia walemavu hapa nchini. Hoja hii inapendekeza vijana wa nchi hii wajimudu kimaisha. Mwaka wa 1976, Shirika la October 26, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 3201 Leba Ulimwenguni yaani, ILO, ilianza kuisaidia Wizara hii. Walemavu walinunuliwa cherehani na kufunzwa jinsi ya kujitegemea. Ijapokuwa usaidizi huo haukutekelezwa kikamilifu, ilikuwa ni ishara nzuri. Pesa nyingi zilizokusanywa hazikuweza kuwafaidi hawa watu. Juzi kulikuwa na Swali hapa Bungeni kuhusu matumizi ya pesa zilizokusanywa wakati wa utawala uliopita ili kuwasaidia walemavu. Pesa hizo zilitumiwa kununua nyumba. Je, nyumba hizo zinawafaidi walemavu kwa njia gani? Je, pesa hizo ziko wapi? Pesa nyingi zinazotumika katika Wizara hii zinatoka kwa wafadhili. Kwa hivyo, tunafaa kuhakikisha kwamba pesa hizo zinatumika kwa njia nzuri ili ziweze kuhudumia hata vizazi vijavyo. Wizara hii inabeba mzigo mzito hapa nchini. Kuna idadi kubwa ya vijana nchini. Hivi majuzi kulikuwa na mradi wa kuhimiza upangaji wa uzazi. Wakenya hawataki kupanga uzazi. Wanazaa watoto wengi ili wawe na kura nyingi. Lakini kuwalisha watoto wengi wanaozaliwa ni shida kubwa. Wakati huu, Serikali imetoa elimu ya bure katika shule za msingi. Hao watoto watakapoanza kujiunga na shule za upili, watakuwa wengi sana. Hakutakuwa na shule wala waalimu. Idadi ya waalimu inapungua kwa sababu wengi wanakufa kutokana na maradhi mbali mbali, hasa Ukimwi. Bw. Spika, ni lazima tuwe na mwongozo. Hili Bunge la sasa limejaa wasomi. Tunajua Wizara hii inashughulikia maslahi ya viwete, vijana, wasichana, wanaume, wazazi, michezo na utamaduni wa Kenya. Kwa hivyo, tutafanya nini ili tujimudu? Hilo ni suala ambalo ni lazima tuliangazie. Hatuna nafasi ya kuleta wataalamu kutoka nje waje watufundishe jinsi ya kuishi. Wizara hii ni lazima itilie mkazo upangaji wa uzazi. Kila mtu awe na watoto ambao ataweza kuwatunza, ili tuhifadhi uchumi wetu. Waturkana wanazaa watoto wawili ama watatu na wanawalinda vyema. Ukienda Pwani, utapata mtu mmoja ana watoto 12 na ilhali, hana shamba! Chakula chake ni wali tu! Hapati kunde! Anategemea kunde kutoka bara. Kuna wakati Wizara hii ilitangaza kwamba mtu akiwa na mtoto kiwete, asimfiche nyumbani; amlete huyo mtoto ahudumiwe, kwa sababu ni mwanadamu pia. Wengi waliletwa na sasa, tuna hata shule ya vipofu huko Thika. Jukumu hilo lilichukuliwa na dhehebu la Jeshi la Wokovu. Walizingatia kwamba kipofu pia ni mwanadamu. Walileta sera mpya kwamba kipofu anaweza kufundishwa na akasoma. Leo hii, kuna vipofu ambao ni wahadhiri wa vyuo vikuu na wana shahada sambamba na wale ambao wako na macho. Tunapaswa kuwapa hongera wamishenari ambao walileta huo utaratibu. Sisi tunakaa tu kama walinzi wa lango. Tunapokea tu! Je, tuna jukumu gani katika kulijenga hili taifa letu?"
}