GET /api/v0.1/hansard/entries/237712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 237712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237712/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, hili taifa ni la watu wote. Tukiangazia mambo ya elimu na uchumi, watu ndio msingi wa taifa hili. Wanaweza kutupatia maisha bora katika siku zijazo. Wahenga walisema: \"Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!\" Wakati nilipofumba hilo fumbo kwa Bw. Ojode, Bunge liliyumbayumba kwa sababu wengi hawajui Kiswahili. Hata Bw. Balala, ambaye anatoka Pwani, Kiswahili chake ni chepe chepe! Hakuweza kufumbua fumbo nililofumba - mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mtoto anatunzwa na wazazi wake na ikiwa hakutunzwa vizuri, tabia yake huwa mbovu. Wanasema elimu ya mtu huanzia nyumbani."
}