GET /api/v0.1/hansard/entries/237715/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 237715,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237715/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Capt. Nakitare",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Wanataka sisi tunaokaa viti vya nyuma tukaze shingo zetu ili twende huko mbele kuomba maji. Mtuwiye radhi tuseme tunayoyajua. Magurudumu ya nyuma ndiyo huendesha gari na wala sio ya mbele. Bw. Naibu Spika wa Muda, Hoja hii ina maana sana kwa sababu inazingatia mambo yatakayokuja baadaye. Tutawezaje kufuata utamaduni, mambo ya jinsia na maendeleo ikiwa hatuna mpango? Mpango wowote Serikalini unaanza na Wizara inayohusika na utamaduni. Namuomba Waziri azingatie mambo hayo. Idara ya Vijana ilitoka kwa hiyo Wizara. Serikali haijasema ni kiwango gani cha pesa za vijana kitaenda kwa viwete na viziwi. Hawana bahati ya kuona mkihesabu pesa hizo. Hawana nguvu ya kwenda haraka ili wafike kwenye meza mnayogawania pesa. Kwa hivyo, Serikali izingatie hayo mambo kupitia kwa Wizara hii. Kuna watu ambao wanahusishwa na wasiojiweza. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}