GET /api/v0.1/hansard/entries/237723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 237723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237723/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kajembe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 163,
        "legal_name": "Ramadhan Seif Kajembe",
        "slug": "ramadhan-kajembe"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa pia kutoa maoni yangu juu ya Hoja hii, haswa tunapozungumzia usawa wa jinsia. Bw. Naibu Spika wa Muda, kitu ambacho ningetaka kiangaliwe kwa makini na Serikali, na hasa Wizara inayohusika, ni zile harusi zinazofanywa kwa wasichana wadogo. Utaona katika beaches zetu, watalii wanaokuja, wengine hawana nidhamu kwa sababu huchukuwa watoto wadogo kutaka kufanya mapenzi nao. Nafikiri mambo kama hayo yanatakikana yaangaliwe na yasimamishwe. Bw. Naibu Spika wa Muda, Serikali yetu pia ingefikiria kwamba harusi za mapenzi zinafanya watoto wasipate elimu. Yaani, kwa vile tunataka jinsia watu wote wawe sawa, wake kwa waume, utakuta kwamba wasichana wakiolewa mapema wanakosa elimu. Nasi tunasema kwamba vile wanaume wanavyopata elimu, iwe hivyo hivyo na akina mama nao wapate elimu kama vile waume. Yaani, tunataka maendeleo ya namna hiyo. Kuhusu mambo ya kugawanya kazi katika nchi, au mambo ya kupigania viti vya siasa, mpaka sasa sidhani kama akina mama wamezuiliwa wasipiganie viti vya siasa. Kwa hakika wanapigania. Wako na wanachaguliwa kama wanaume. Nao pia wanaingia Bungeni. Wanaingia katika mabaraza ya miji. Kitu ambacho ni muhimu ni wakati uliopita jamii nyingine katika nchi hii walichukilia kwamba ilikuwa si muhimu kuelimisha wasichana. Mimi hufikiri jambo la kuelimisha wasichana lataka lifanywe sambamba na vile ambavyo wavulana wanaelimishwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi nataka niseme hivi: Juu ya mambo ya kupigania viti vya siasa, sidhani hapo kwamba kuna kitu jinsia itaingia kati kwa sababu hakuna mwanamke aliyekatazwa kupigania kiti cha siasia. Ni juu ya mwanamke mwenyewe apige kampeini yake. Tumeona wanaume wakiangushwa kisiasa na wanawake lakini juu ya wao kupewa kazi na Serikali, nafikiri hiyo nataka ifanywe sambamba na wale ambao wamepata masomo ya juu ambao wanaajiriwa kazi na Serikali. Hakuna haja ya akina mama kujiona ni wanyonge. Wao ni binadamu kama wanaume lakini nataka niseme kuna mambo mengine ya kimila. Pia kuna mambo mengine ambayo yameletwa na dini. Mpaka sasa tukiwa Waafrika na tukiwa watu wa madhehebu ya dini tofauti, mpaka sasa tabia zinasema mwanamume ndiye atakayemuoa mwanamke. Sidhani kama itakuja siku ambapo mwanamke atamuoa mume. Siku hiyo ikija itakuwa ni hali ya mshangao. Unajua pia kuna 3206 PARLIAMENTARY DEBATES October 26, 2006 madhehebu ya dini yanayoruhusu watu kuoa mpaka wake wanne. Hiyo inakaribishwa kwa kulingana na madhehebu ya dini kwa sababu Katiba ya nchi hii imesema uhuru wa kuabudu utawekwa maanani na utashikiliwa kisawasawa. Mambo kama hayo ya mume kuoa mke na mwanamume kuoa wake wawili, watatu au wanne, ni ya wanaume na sidhani kama hapo tuna usaidizi wowote tuweze kuambia akina mama \"sasa na nyinyi muoe waume wawili, watatu au wanne\". Nafikiri hapo itakuwa ni vigumu sana."
}