GET /api/v0.1/hansard/entries/237725/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 237725,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237725/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kajembe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 163,
"legal_name": "Ramadhan Seif Kajembe",
"slug": "ramadhan-kajembe"
},
"content": "Itakuwa ni miujiza! Kwa hiyo, ingawaje akina mama wanataka wapewe haki sawa na wanaume, lakini wajue kwamba kuna haki nyingine ambazo ni za wanaume tu. Wakiziingilia, hawaingii. Kwa mambo mengine ulimwenguni, hayo ni sawa kwa sababu leo tuna wanawake wanaoendesha ndege, kuna wanawake ambao wanaenda mwezini, yaani astronauts, na wako katika mambo mengi na hakuna ambaye anawazuia mambo hayo. Akina mama ni mama zetu waliotuzaa na lazima tuone kwamba wanaenda mbele, lakini nao pia wasaidie kwamba zile arusi za mapema kwa wasichana ziwe zimeondoka kabisa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kitu ambacho labda niseme ni wakati mume na mke wako nyumbani, kiafrika mume ndio mwenye hapo lakini kuna mama wengine wanajifanya waume nyumbani. Sasa inakuwa ni matatizo. Lazima tukubaliane kwamba wanaume wakiwa nyumbani na akina mama, wao ndio wenye kushikilia nyumba na mama naye anakuwa kama msaidizi wa yule mwanamume. Mambo ya mwanamke kusema: \"wewe bwana kaa chini\", ama \"bwana nenda sokoni\" si kiafrika. Kwa hivyo, ingawaje tunazungumzia mambo ya jinsia, pia tusisahau kwamba tukiyazungmza mambo ya jinsia, tusitoke katika mila na dini zetu. Nataka kusema kwamba mwanamume ameumbwa kuwa na imani sana. Mwanamume kwanza ana imani na mke wake. Mwanamume ana imani na watoto wake, ingawaje saa nyingine ukioa wanawake wawili au watatu, wanakuwa na wasiwasi. Wanafikiri ni nani anapendwa zaidi. Mwanamume anapenda wale wanawake wote aliowaoa kwa usawa kabisa. Ingawaje wengine wanakuwa na wasiwasi eti \"si tumeolewa watatu au wanne, ni nani ana mahaba zaidi na huyu bwana\"? Kama huna mahaba na yeyote pale, hungemuoa. Kwa hiyo, pia akina mama na mabibi waondoe wasiwasi na wajue bwana akioa wawili, watatu au wanne, bwana huyo ana mahaba na hao wote na atawatunza. Ni wake zake. Ana imani nao. Atazaa nao na watoto watakuwa ni wa huyo bwana na hao mabibi. Bw. Naibu Spika wa Muda, basi, nami naunga mkono Hoja hii."
}