GET /api/v0.1/hansard/entries/237791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 237791,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/237791/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Spika, kazi tunayoifanya sasa, ya kuchagua Wabunge watakaotuwakilisha katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni nzito mno. Naijua kwa sababu niko katika Kamati ya Mashauri ya Nchi za Nje na Ulinzi. Tumeshughulikia sana mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mimi sitazungumza mengi. Lakini jambo ambalo naomba kusema ni kwamba, pamoja na sheria zote, ziwe za kidemokrasia au la, Serikali ina jukumu muhimu la kuhakikisha kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki inalindwa na kwamba, Wabunge wanaoenda huko wana baraka za watu wote wa Afrika Mashariki. Tukiangalia vyama vyote, hasa chetu cha FORD(P), watu wote wanatoka sehemu moja. Hiyo haionyeshi haki hata kamwe. Jambo la mwisho, tukiangalia swala la majimbo, watu wa Pwani wameachwa---"
}