GET /api/v0.1/hansard/entries/238016/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 238016,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/238016/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Spika, hilo jibu ni la kusikitisha kabisa, hasa kwa walimu wa Wilaya ya Taita-Taveta. Ni jibu ambalo lina lengo la kuendeleza vurugu na kuvunja motisha wa kufundisha kwa walimu wa Taita-Taveta. Waziri Msaidizi amesema kuwa tume ya kuwaajiri walimu ilifanya utafiti na ikatoa ripoti yake. Tarafa ya Taveta ndiyo yenye hali ngumu zaidi katika Wilaya ya Taita Taveta. Tarafa ya Wundanyi inapakana na tarafa za Mbololo, Mwatate na Voi, ambako walimu wanapata pesa za kufanya kazi katika mazingira magumu. Shule kama Kishushe, Ngongodinyi, Sagenyi, Sirienyi na Mwoloko ziko katika mazingira magumu zaidi. Je, ni vigezo gani vilitumiwa na Wizara ya Elimu katika kuamua kwamba katika Wilaya ya Taita-Taveta, walimu kutoka Mwatate, Voi na Mbololo watapata pesa za kufanya kazi katika mazingira magumu na kuwaacha walimu kutoka Wundanyi na Taveta?"
}