GET /api/v0.1/hansard/entries/238080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 238080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/238080/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Capt. Nakitare",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii 3122 PARLIAMENTARY DEBATES October 25, 2006 ambayo inalenga maendeleo ya Kenya. Kutoka wakati nchi hii ilipopata Uhuru kutoka kwa wakoloni, mfanyabiashara wa Kenya hakuangaziwa kama mtu ambaye ana faida kwa maendeleo ya Kenya. Kuna wachuuzi ambao wamekuweko kwa miaka mingi. Kabla hawa wachuuzi wa bidhaa ndogo ndogo kuja miaka ya juzi, biashara ile ambayo Mwafrika alikuwa anajulikana kufanya, ilikuwa kuweka cherehani mbele ya duka la Mhindi ili aweze kufanya kazi hiyo. Hicho ndicho chanzo cha biashara ya wachuuzi. Mifano mingi imetolewa kuambatana na kujimudu kwa watu wa Kenya. Ninashangaa, kwa sababu Wizara ya Biashara na Viwanda inazingatia maslahi ya matajiri. Mtu akija kutoka nje anasema kuwa anataka kuweka rasilmali yake na kuwa ana mamilioni ya dola. Anapewa kiwanja na kuambiwa: \"Karibu. Wewe ndiye mkubwa\". Je, mtu huyu anakuja kutunyonya au kutuletea faida? Ingetufaidi kama angeanzisha kiwanda kwa minajili ya kuajiri watu. Hakuna sehemu katika Wizara hii inayopata pesa kutoka kwa wenye kutoa kodi. Hii Wizara haijawasaidia wachuuzi."
}